Rania Nasser ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano ameandaa maonyesho ya picha yanayojulikana kama ‘Watu wa Tanzania’ ambayo yatafanyika Alliance Francaise jijini Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Agosti 2020.
Matumizi ya picha na video kuelezea stori au hadithi ni muhimu Sana, yanaelimisha, kubadilisha Habari za kihadithiwa na muonekano pamoja na kuleta mabadiliko chanya kwa Dunia. Tumeona mfano mingi kwenye hili. Mabadiliko yanaanza kwa kubadilisha maono ya jamii.
Tangu akiwa na umri mdogo, Rania ametembelea sehemu mbali mbali za nchi yake Tanzania na sehemu zote hizo ambazo ametembelea na watu aliokutana nao, na Habari zile ambazo amezipata, ameona kilicho bora kwa Watanzania.
Rania pia ameweza kutembelea nchi zingine ulimwenguni lakini ukarimu na upole wa Watanzania umekuwa ni wa kipekee.
Wakati wa kutembelea nchi hizo zingine, Rania ametengeneza marafiki wengi. Kitu kimoja ambacho ameweza kutambua ni kwamba wengi wanajua machache kuhusu Bara la Afrika, na Sana Sana Tanzania. Anasema ‘naelewa ya kwamba kuna watu hawajui ya kwamba Afrika sio nchi, na hii sio kwa kila mtu, siwezi kupata picha kwa umasikini unaokumba vijiji vyetu, mapigano kwenye Miji yetu, magonjwa na mengine mengi’