…………………………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM )mkoani Pwani kimewaasa baadhi ya wanachama wake kuondoa makundi na kuacha kuwekeana chuki badala yake waungane kuwa wamoja na kushikana baada ya uchaguzi wa ndani kukamilika .
Kimeeleza ,kwasasa hatua mbalimbali zitaendelea na vikao vya maamuzi ya kuteua wagombea watakaopeperusha bendera katika uchaguzi mkuu unaokuja hivyo haina budi kuwa watulivu na upendo .
Akielezea mchakato wa uchaguzi walivyojipanga baada ya hatua za awali za chama kukamilika ,katibu wa CCM mkoani Pwani ,Anastazia Amas alisema mkoa umejidhatiti kushinda kwa kishindo chaguzi nafasi ya Urais,wabunge na madiwani.
Alieleza ,haina ubishi mchakato wa kura za maoni umeenda kidemokrasi hivyo kilichobakia sasa ni kuwa wamoja .
“Chuki na visasi kwasasa havina nafasi ,wanachama wawe pamoja ,sio kama wapo wanaowekea chuki bali katika uchaguzi wowote hakukosekana makundi lakini sasa vitendo hivyo vifikie kikomo:”alielezea Amas .
Amas alifafanua, hatua za uchukuaji wa fomu ulikuwa wa kidemokrasia ,wanachama walijitokeza kwa wingi kuanzia ubunge wa majimbo Tisa na ubunge viti maalum,madiwani.