Home Mchanganyiko NEC yakutana na Vyama vya Siasa na Kutangaza Kuanza kwa Kampeni

NEC yakutana na Vyama vya Siasa na Kutangaza Kuanza kwa Kampeni

0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage akisikiliza hoja za wawakilishi wa vyama vya siasa leo Agosti 1,2020 katika ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika jijini Dar es salaam Jaji Kaijage pia ametangaza kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu,kwamba zitaanza Agosti 26 mwaka huu na kumalizika Oktoba 28 ,2020 kwa upande wa Tanzania Bara.

……………………………………………………

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC)imekutana na Vyama vya Siasa ambao ni wadau Wakuu wa uchaguzi ili kupeana taarifa na kufahamishana kuhusu maandalizi ya Uchaguzi .

Kikao hicho muhimu kwa mstakabali wa nchi yetu kimelenga katika kuelekea Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Oktoba 28 mwaka huu.

Akitoa hotuba hiyo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu .J.K.Nyerere Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Semistocles S.Kaijage amesema katika uchaguzi huo kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura.

“Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,hakukuwa na marekebisho katika Sheria za Uchaguzi ,hata hivyo tume imefanya maboresho ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 ,” anasema Jaji Kaijage.

Anasema NEC imekuwa imekuwa ikiwashirikisha wadau wa uchaguzi katika hatua mbali mbali za mchakato wa uchaguzi mathalan kabla ya kuanza zoezi la uboreshaji ,Tume ilifanya maboresho ya Kanuni ambapo ilikutana na Vyama hivyo vya Siasa na kupokea maoni yao.

Aidha Mach,2019 na 4 Aprili mwaka huu tume ilivitaarifu Vyama kuweka Mawakala wakati wa zoezi la uboreshaji.

NEC imepambanua kuwa kupitia vyombo mbali mbali vya habari ratiba ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu ambapo serikali imetoa tamko siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko .

Ratiba juu ya uchukuaji wa fomu za uteuzi zitaanza kutolewa August 5, 2020 kwenye makao Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi jijini Dodoma kwa wagombea wa kiti cha Rais .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Mahera Charles amesema kuwa wagombea Ubunge na Udiwani zitatolewa kwenye Makao Makuu ya Halmashauri yalipo Majimboni na Kata husika kuanzia Augusti 12 hadi Agusti 25 mwaka huu.

Almesema ratiba kipindi cha uchaguzi ,kipindi cha kampeni za uchaguzi kitaanza Agusti hadi Oktoba 2020 kwa upande wa Tanzania Bara kwa upande wa Zanzibar kampeni hizo zitaishia Oktoba 26 ilikupisha upigaji wa kura

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt Wilson Mahera akionesha moja ya kijarida chenye maelekezo mbalimbali kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage akijadiliana jambo na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Asina Omary wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam

Kutoka kulia ni Msajiri wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Saisa Bw. John Shibuda wakiwa katika mkutano huo.

Katibu wa (NEC) Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole akizungumza jambo katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye kikao hicho .