Ofisa Uchechemuzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Florence Majani akizungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari za jinsia. Mwezeshaji wa Mafunzo Wakili na Mwandishi wa Habari Mary Mwita akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha yaliyofanyika jijini Dodoma jana. Ofisa Uchechemuzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Florence Majani akizungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha wakati wa mafunzo kuhusu nafasi yao kwenye kusaidia jamii kutambua dhana nzima ya jinsia na usawa hasa kwa wanawake wanaoshiriki siasa nchini. Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya siku moja yalitolewa na TAMWA jana jijini Dodoma. Waandishi wa habari wakifuatilia kwa karibu mafunzo kuhusu nafasi yao katika kuandika habari za jinsia na usawa hasa kwa wanawake wanaoshiriki siasa.
********************************
NA SULEIMAN MSUYA
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimewashauriwa waandishi wa kuandika habari za jinsia ili kuhakikisha lengo kuwepo usawa wa kijinsia linatimia nchini.
Ushauri huo umetolewa na Ofisa Uchechemuzi wa TAMWA, Florence Majani wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari zaidi ya 20 kutoka katika mikoa ya Arusha na Dodoma ambao wapo katika Mradi wa Wanawake Sasa unaofadhiliwa na Mfuko wa African Women Development (AWDF).
Majani alisema pia mradi huo unahusisha waandishi wa mikoa ya Dar es Salaam na Zanzibar ambapo wanaamini kundi hilo ni muhimu katika kufikia jamii hasa wanawake kuhusu ushiriki wao katika shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi bila kuwa na hofu ya jinsia yake.
Alisema kupitia mafunzo hayo waandishi wataweza kuhabarisha taarifa za ushiriki wa wanawake katika chaguzi, changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli za kisiasa.
“Mafunzo haya yanalenga masuala yote ya uchaguzi kama sheria, changamoto na mengine hivyo wanahabari wakijengewa uwezo watakuwa na upeo mkubwa wa kuandika habari hizo kwa kina na ufanisi,” alisema.
Aidha, alisema wanawake wanasiasa wamekuwa wakipitia changamoto kama rushwa ya ngono, matusi, uchumi duni na nyinginezo hivyo watu sahihi wa kusaidia ufumbuzi huo ni waandishi wa habari.
Alisema vyama vya siasa ni chanzo kushindwa kupitisha wanawake kugombea nafasi za uongozi kutokana na changamoto ya rushwa ya ngono na udhalilishaji.
Majani alisema baadhi ya wanawake wamekuwa hawana nafasi kwenye siasa na katika ngazi za maamuzi hivyo ni vema juhudi za waandishi kuripoti hayo zikaongezeka.
Ofisa Uchechemuzi huyo alisema yapo mambo mengi yanayojitokeza katika kushindwa kwa wanawake kwenye uchaguzi zikiwemo gharama za uchaguzi, mfumo dume unaosisitiza uongozi wa kaya tangia awali, udhalilishaji katika uchaguzi na mfumo mzima wa uchaguzi.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku moja Muwezeshaji, Wakili Mary Mwita alitaja ana za udhalilishaji wa kijinsia kuwa ni pamoja na shambulio la mwili, rushwa ya ngono, udhalilishaji wa kisaikolojia na uchumi duni.
Mwita alisema usawa katika uchaguzi umeainisha mapengo ya jinsia katika sheria tano kwa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia kwamba ni pamoja na kutokubaguliwa kwa njia yeyote ile kwenye mchakato wa uchaguzi, haki ya kupiga kura, kuteuliwa, haki ya kufikia na kutumia rasilimali za uchaguzi, kuhabarishwa na kusikilizwa na haki ya kuchaguliwa.
Aliwataka waandishi wa habari kutoa taarifa kuhusu manyanyaso juu ya wanawake sambamba na kujielimisha kuhusu masuala ya jinsia na kuzifahamu sheria zinasemaje kuhusiana na maswala ya jinsia, pamoja na kuchambua masuala ya jinsia katika jamii.
“Katiba ya Tanzania kuanzia Ibara ya 12 hadi 29 inazungumzia haki za binadamu kama haki ya kuishi, usawa kwa watu wote, haki ya kumiliki mali, kila mtu ana haki sawa mbele ya sheria na hatakiwi kubaguliwa na haki nyingine muhimu.
Tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainishwa msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2) kinakariri kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsi lugha na itikadi za kisiasa,” aliswma
Aidha, alisema mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake 1979 unasisitiza kwamba ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.
Wakili Mwita alisema, ngazi ya kanda maridhiano ya mkataba mwaka 2000 iliingizwa na kubainishwa misingi ya usawa wa jinsia katika kifungu cha 4(1) katika makubaliano yaliyofanyika mwaka 2000
Alisema tamko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC2005) liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake katika kuwa asilimia 30 na baadae kupandisha hadi kufikia 5O hali ambayo Tanzania haijafikia kwa sasa.
Mwita alisema ushirikiano baina ya makundi mbalinbali na taasisi za zinazoshikiana tunawe kupaya matoke chanya ya kiuchumi na kisiasa.