Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza leo Jijini Dodma katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali, Charles Mbuge, akisoma taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa jengo hilo..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akisalimia katika sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage akitoa neno katika sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa nchini waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifatilia sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe katika Uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la Ndejengwa Jijini Dodoma.“
PICHA NA ALEX SONNA
………………………………………
Na.Majid Abdulkarim, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametoa siku 14 kwa taasisi na mashirika yanayodaiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA GUARD) kuwa wamelipa madeni hayo ili kuliwezesha jeshi hilo kutekeleza miradi kikamilifu.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dodma katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kila taasisi iwe ya serikali au binafs ndani ya siku 14 kila tasisi kuwa imelipa deni lake na kupewa listi kuwa wamelipa na JKT.
Rais Magufuli ametoa wito kwa viongozi wa siasa nchini kuendesha kameni zao kwa ustarabu, kunadi sera zao bila kutoa kauli chafu na kutanguliza uzalendo kwa kulinda amani na kuufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa maalumu.
“Katika siasa zetu tujitahidi kunadi sera zetu kwa kumtanguliza mungu lakini pia tujenge hoja wakati wa kuwasilisha sera zetu kwa wananchi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi kujua yupi kiongozi sahihi anawafaa pale itakapo fika 28 Oktoba, 2020 siku ya Uchaguzi Mkuu.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameiongezea Tume ya Taifa ya Uchaguzi Milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha vifaa muhimu vinavyotakiwa katika jingo hilo ili kuweza kutekeleza shughuli zake ipasavyo.
“Lakini pia vifaa vilivyopo katika ofisi zilizokuwa Dar es Salaam pia mviamishie huku ili kuweza kurahisisha sghuli zenu na kuleta ufanisi mzuri katika utendaji kazi wenu” amesisitiza Rais Magufuli.