Home Makala FABRICE MUAMBA NA DAKIKA 78 ZA MSTARI WA KIFO NA UHAI NDANI...

FABRICE MUAMBA NA DAKIKA 78 ZA MSTARI WA KIFO NA UHAI NDANI YA NORTH LONDON

0

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Nani anakumbuka jioni ile ya michuano ya FA CUP ndani ya dimba la White Hart Lane mwezi March 2012, mtanange kati ya Tottenham na Bolton, Nani anakumbuka Ile dakika ya 43 ya mchezo, nani anakumbuka majonzi ya Jim Beglin, Nani anakumbuka simanzi kubwa pale London ya Kaskazini?

Wakati Muamba akionekana amedondoka kama mti, ni ghafla sana fundi wa Uholanzi Rafael Van De Vaart akasogea pale na kuita madokta wasogee kutoa support ya haraka, Muamba hapumui Wala hatikisiki, nafsi imesimama, kila kitu kimetulia, Ni Vita kubwa Kati ya Malaika mtoa roha na nafsi ya Muamba.

Bahati iliyoje hiyo siku Spurs walikuwa na madktari wengi, bwana Shabaaz Mughal, Peter Fischer na Wayne Diesel, wakati Bolton walikuwa na Andy Mitchell na Jonathan Tobin, kwa haraka waligundua ni Cardiac arrest, wakaambiazana hatupaswi kupoteza hata sekunde wakatumia Cardiopulmonary Resuscitation (CPR) kwa ajili ya kuongeza Oxygen, hii husaidia kupunguza hatari kwa 10%

Wakati Vita kubwa kati ya nafsi ya Muamba, madaktari dhidi ya Malaika mtoa roho, kulikuwa na shabiki mmoja Andrew Deaner, huyu Ni daktari aliyebobea kwenye moyo ‘cardiologist’ akawageukia rafiki zake akasema ‘i need to help them’ naomba nishuke nikapambane na wenzangu tumuokoe.

Wakati Deaner anashuka walinzi walimkataza, ghafla Babu mmoja nae mlinzi alimruhusu pita nenda Daktari, nenda kampambanie kijana, wakati Deaner anafika pale aliwaambia tuendeleze hizi shoti tunazompiga ‘defibrillation shocks’ tupige nyingi ili tumuokoe, Deaner dakika chache alikuwa shabiki Ila sasa Ni Daktari kiongozi, aliyebobea kwenye fani yake.

Wakati Fabrice anatolewa uwanjani, mashabiki wamesimama wanaimba ‘Come on Fabrice’ wote kwa pamoja, wakati huo wachezaji wanalia, wakati wanaingia kwenye gari ya wagonjwa, kwa haraka inapasua njia ya North London kwa Kasi mno, Dr. Dreaner kwa haraka aliwaambia, tumpeleke London Chest Hospital na sio Middlesex kwakua yeye anafanya kazi pale.