Home Mchanganyiko TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU,NI OKTOBA 28 2020

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU,NI OKTOBA 28 2020

0
Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage akizungumza wakati akitangaza ratiba ya uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 28 2020 nchini kote.
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) nchini Tanzania imesema, Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na Urais wa Tanzania utafanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020, Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage amesema Uchaguzi mkuu utafanyika October 28 Mwaka huu huku Kampeni zikitarajiwa kuanza August 26 hadi October 27, 2020.
Wakati huo huo Uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Urais,Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani utafanyika August 25, 2020