Home Siasa NEC YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI

NEC YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI

0
……………………………………………………………………………..
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) nchini Tanzania imesema, Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na Urais wa Tanzania utafanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne tarehe 21 Julai 2020, Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage amesema Uchaguzi mkuu utafanyika October 28 Mwaka huu huku Kampeni zikitarajiwa kuanza August 26 hadi October 27, 2020.
Wakati huo huo Uteuzi wa Wagombea wa kiti cha Urais,Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani utafanyika August 25, 2020

TAARIFA KWA UMMA 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 41(4) ya 

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa 

pamoja na vifungu vya 35B (1), (37) (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya 

Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 48 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya 

Serikali za Mitaa, Sura ya 292, inapenda kuutarifu Umma kuwa Ratiba ya 

Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani wa 

Tanzania Bara itakuwa kama ifuatavyo- 

NA TUKIO TAREHE 

  1. Uteuzi wa Wagombea wa Kiti cha Rais 

na Makamu wa Rais, Ubunge, na 

Udiwani 

25 Agosti, 2020

  1. Kampeni za Uchaguzi Kuanzia 26 Agosti, 2020 hadi 

27 Oktoba, 2020 3. Siku ya Uchaguzi 28 Oktoba, 2020 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 

Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst.) Semistocles S. Kaijage 

MWENYEKITI 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 

21 Julai 2020