………………………………………………………………………..
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.
Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA [21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.
Leo tarehe 18.07.2020 majira ya saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
WITO:
Ninatoa wito kwa jamii kutofumbia macho ugomvi unatokea mbele yao kwa kudhani ni kitu cha kawaida na kukaa kimya, ni wito wa Jeshi la Polisi kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa Watendaji wa Kata au Wenyeviti wa Mitaa ambao ni walinzi wa amani katika maeneo yao ili waweze kuchukua hatua za awali kupitia baraza la usuluhishi la Kata au Mtaa.
KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia DICKSON KABUJE [32] Mkazi wa Ikumbi akiwa na mali mbalimbali za wizi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 14:00 Mchana huko Kijiji cha Ikumbi, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya na katika upekuzi alikutwa akiwa na mali za wizi ambazo:-
- Spika kubwa 02,
- Redio Sub-Woofer 01 na Spika zake,
- Stablizer 01, m
- Mtungi mkubwa wa gesi Mihani 01,
- Deki 02 za Singsung,
- Godoro 01 Super Banco.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.