Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu Julai 16 amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea ubunge katika Jimbo hilo kwa Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi Norbert Kibaji huku akisema dhamira yake ni kumalizia kazi aliyoanza kipindi cha miezi tisa cha utumishi wake jimboni humo.