Home Siasa WANACHAMA 221 CCM WACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE KATIKA MAJIMBO TISA MKOANI PWANI...

WANACHAMA 221 CCM WACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE KATIKA MAJIMBO TISA MKOANI PWANI -AMAS

0

*********************************

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 221 wamejitokeza kuchukua fomu ya ubunge katika majimbo tisa mkoani Pwani pamoja na nafasi mbalimbali za ubunge viti maalum.
Kati ya hao ,wanachama zaidi ya 175 ni fomu za ubunge wa majimbo ikiwemo 37 Jimbo la Bagamoyo kuchukua fomu za kuwania ubunge , akiwemo aliyemaliza muda wake Dkt. Shukuru Kawambwa huku Jimbo la Chalinze wakiwa wamefikia 23 hadi sasa na Ridhiwani Kikwete akiomba ridhaa kugombea kwa kipindi kingine .

Zoezi hilo lililoanza Jumatano ya Julai 14, wanachama hao wamechukuwa fomu hizo tayari kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho zinazotarajia kufanyika Julai 20 na 21.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu wa CCM Pwani ,Anastazia Amas alisema ,jimbo la Kibaha Mjini 39, Rufiji 26, Kibaha Vijijini 25, Kibiti 11, Mafia 7, Mkuranga 8 na Kisarawe wanne .
“Nafasi za Viti Maalum wako 46 ambapo uwakilishi wa Mkoa wako 19, Wafanyakazi 3, Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO 1, Watu wenye Ulemavu 1 na Wasomi 1,” alisema Amas.
Alieleza, kwa upande wa Vijana wako 16 na Wazazi wanne ambapo zoezi hilo litamalizika Julai 17 mwaka huu.