Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara katika eneo la mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma unaoinguanisha Tanzania na nchi Jirani ya Msumbiji. Ziara hii inalenga kibaini na kutatua changamoto mbalimbali ili kukuza biashara na uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji. Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololet Mgema. Akiwa mpakani hapo Dkt. Ndumbaro amefanya mazungumzo na watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali walipo katika ofisi za mpaka huo kwa lengo la kusikiliza changamoto na mapendekezo yanayolenga kuboresha namna ya utoaji huduma kwa wakazi wa eneo la mpaka na watumiaji wa mpaka huo. Aidha, Dkt. Ndumbaro pamoja na kutoa ufumbuzi wa baadhi ya changamoto, na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizosalia amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu, jitihada na uaminifu. Dkt. Ndumbaro pia ametembelea Ofisi za mpakani kwa upande wa Nchi jirani ya Msumbiji na kufanya mazungumzo na Watumishi walipo katika Ofisi hizo. Mheshimiwa Ndumbaro, amewaleza wakazi na watumishi walipo mpakani humo kuwa Serikali inanendelea na hatua za kuzitatua changamoto kubwa zinazo changia ugumu wa utekelezaji wa majukumu ya kilasiku na kuadhiri mwenendo wa biashara mpakani hapo, ikiwemo ukosefu wa umeme, huduma ya mawasiliano na barabara ya kiwango cha lami. Dkt. Ndumbaro amewapongeza Watumishi walipo mpakani kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewahimiza Watumishi hao kuendelea kutekeleza Dilomasia ya Uchumi, kuendeleza uhusiano mwema na kushughulikia suala la Diaspora
|