Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chekelei korogwe mkoani Tanga wakimsikiliza mkufunzi wa masuala ya jinsi na jinsia . Wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Bungu ambao wanakaa bweni wakielekea darasani kwa ajili ya masomo ya ziada.Wanafunzi wa shule ya msingi Chekelei wakiwa katika michezo wakati wa mapumziko.
******************************
Na Mwandishi Wetu Korogwe
Idadi kubwa ya Wanafunzi wilayani Korogwe wamesema kuwa mpango wa elimu kwa Masafa ya Radio na Televisheni au kuwasaidia wakati wa likizo ya Corona kutokana na mazingira yanayowazunguka na umaskini ambao unapelekea kaya nyingi kutomiliki vifaa hivyo vya kielectroniki.
Hayo yamesemwa na wanafunzi mbalimbali wilayani hapa, Simoni Shehondo ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Wilayani korogwe Katika shule ya sekondari ya Mlungui anataja kuwa wakati wa likizo walitumia muda mwingi shamba na sio kusikiliza Radio kwa ajili ya kujisomea.
” sisi kwetu hatuna televisheni na Radio ni ya baba muda wote anakuwa nayo yeye atakama atakuwa amekwenda Wana chai hivyo Mimi sikupata muda kabisa wa kujifunza kupitia radio na TV” anasema Simon
Anasema muda mwingi tulikuwa tunautumia kwenye kucheza na kusaidia kazi za nyumbani hivyo mfumo huu wa radio aujatusaidia kabisa.
Nae Almisha Issa Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari mlangai anataja kuwa wakati wa likizo watoto wa kike walipata changamoto kubwa ya kurundikiwa kazi na wazazi Wao.
“Sisi uku kwetu mtoto wa kike ndio anaenda shambani, ndio huyo aandae chakula cha familia hivyo kazi zilikuwa nyingi kiasi kipindi chote cha likozo nilishindwa kugusa hata daftari”Anasema Almisha.
Nae mwalimu mlezi wa shule ya sekondari Bunch, Edda Mgaya anasema kuwa wamewauliza wanafunzi wao Kama walipata nafasi ya Kusoma na kupitia baadhi ya mada kwa njia ya Radio wamegundua hakuna hata mmoja.
“Maisha huku ni tofauti sana na mjini kwani vijana wengi wa kiume walikuwa wanakaa vijiweni na watoto wa kike kazi za Nyumbani jambo ambalo liliwafanya wakasahau kama kuna shule tena” anasema Mwalimu Mgaya.
Kwa upande wake Mwalimu, Josephine Mhina Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Chekelei alitaja kuwa wanafunzi wake wamekuja shule Kama wanaanza upya hivyo hakuna mazingira yanayoonyesha kuwa kulikuwa na mtoto anajifunza nyumbani kwa njia yoyote ile.
Anasema asilimia 90% ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu wengi wao walikuja na madaftari mapya pindi shule ilipofungua.
Ukitazama huku familia nyingi ni maskini Kama hiyo televisheni watoto uangaliaga kwenye mabanda ya mpira na wakati wa corona mabanda yote yalifungwa .