Home Siasa Habibu Mchange achukua fomu kuwania Ubunge Kibaha Mjini

Habibu Mchange achukua fomu kuwania Ubunge Kibaha Mjini

0

Mkurugenzi wa kampuni ya Ador Tanzania Ltd, Habibu Mchange akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuchukua na kurejesha fomu Leo. Mkurugenzi wa kampuni ya Ador Tanzania Ltd, Habibu Mchange akikabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha.Mkurugenzi wa kampuni ya Ador Tanzania Ltd, Habibu Mchange akirejesha fomu ya kuwania Ubunge jumbo la Kibaha Mjini.

***************************************

Na Mwandishi Wetu,Kibaha

Mkurugenzi wa Kampuni ya Ador Tanzania Limited inayochapisha magazeti ya Jamvi la Habari na Times Observer, Habibu Mchange Leo amechukua na kurudisha fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Kibaha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Mchange amechukua na kurudisha fomu hiyo majira ya saa tisa mchana akiwa ameongozana na mkewe Zaria Abdalah Mchange .
Akizungumza Mara baada ya kurejesha fomu hiyo mchange amesema kuwa amechukua fomu hiyo kutimiza haki yake ya kikatiba Kama Mwanachama wa CCM.
“Nimechukua fomu Leo Kama haki yangu ya Kikatiba inavyonitaka hivyo mengine mengine yote tuwaachie vikao wao ndio watahamua” anasema Mchange.