Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuhuma zilizokuwa zinakabili aliyekuwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde .
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya TAKUKURU Mkoa wa Dodoma kumsafisha kwa kudai kuwa hakuna ushahidi wa Mbunge huyo alitoa rushwa.
……………………………………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema kuwa hadi sasa haijafanikiwa kupata vithibitisho kwa aliyekuwa mbunge wa Mtera Livingstone (kibajaji) Lusinde na mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Halima Okashi kuwa walitoa rushwa ya fedha kwa wajumbe.
Naye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde baada ya taarifa ya TAKUKURU ametoa wito kwa wanasiasa kuwa kila kunapotokea changamoto za tuhuma kwao wawe wavumilivu ili kutoa nafasi kwa vyombo husika kufanya kazi yake kwa weledi na badae kutoa taarifa ya uchunguzi wao.
“Kwani kila ukipata tuhuma na wewe ukajibu kwa maneno unaweza leta tatizo zaidi ya hilo ulilokuwa nalo, hivyo wanasiasa na watanzania kwa ujumla kipindi hiki ni wakati sahihi wa kutumia busara katika changamoto tunazokutana nazo hasa katika kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2020”, amesema Lusinde.
Lusinde ameipongeza TAKUKURU wa kufanya kazi kwa weledi na kuja na taarifa sahihi ambayo sasa jamii inaelewa ukweli wa jambo kwa undani zaidi baada ya taairfa ya TAKUKURU kutolewa.
“TAKUKURU wameeleza wazi kuwa hakukuwa na tuhuma yoyote ya rushwa baada ya wao kuridhika katika uchungzi waliyofanya juu yangu”, ameeleza Lusinde.
Lusinde amesisitiza kuwa wanasiasa na watanzania kutoa taaarifa zenye ukweli kwa vyombo vya dola na serikali kwa ujumla ili kutowaumiza watanzania wanyonge katika taifa .