Home Siasa DKT.NDUMBARO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SONGEA MJINI

DKT.NDUMBARO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SONGEA MJINI

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 15 Julai, 2020 amechukua fomu katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Songea Mjini ya Kuomba ridhaa ya CCM kiliwakilisha jimbo la Songea Mjini katika Bunge la Jamhuri yea Muungano wa Tanzania. Dkt. Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake amehudumu katika jimbo hilo kwa kipindi cha miaka miwili baada aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Tutubert Gama kufariki Dunia mwezi Mei, 2020.

Dkt. Ndumbaro aliwasili katika Ofisi ya Wilaya ya Songea Mjini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akitumia usafiri wa Baiskeli na kukadhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi yake ya Ubunge kwa kipindi kingine cha miaka mitano (5) katika uchanguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2020.