Home Siasa MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE BUKOBA MJINI

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE BUKOBA MJINI

0

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), Shabiri Nuah  Bigirwa kushoto akipokea fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini Ndg. Editha Domician kulia ambaye ni katibu wa vijana wilaya ya Bukoba mjini.

………………………………………

Na. Majid Abdulkarim, Bukoba

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), Shabiri Nuah  Bigirwa leo mapema  amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea  Ubunge wa Jimbo  la Bukoba Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Bigirwa amesema kuwa amewahi kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro(MUMSO) na sasa anajitosa katika kugombea Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini.

Bigirwa anasoma Shahada ya kwanza ya Sheria MUM na yuko mwaka wa nne wa kuhitimisha masomo yake.