*********************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MJUMBE wa halmashauri Kuu ya Taifa CCM (MNEC)Pwani, Hajji Jumaa ,amewataka wanachama wa CCM jimbo na udiwani wanaochukua fomu ,kujitathmini kuwa ni viongozi waadilifu,wanaopiga vita rushwa na sio bora kiongozi ambae haendani na mikakati na mipango ya Mwenyekiti Taifa ,Dk.John Magufuli.
Ameeleza watanzania wanahitaji kiongozi anae chapakazi,kujitoa sadaka kwa kusikiliza shida zao na ambae ataacha alama ya kimaendeleo kwenye eneo husika na sio kuondoka kama atakavyoingia.
Akizungumzia masuala ya uchaguzi na michakato inayoendelea ikiwemo kuchukua fomu katika nafasi ya ubunge na udiwani ,Hajji Jumaa alisema ,wananchi na wanaCCM wanatarajia kupata viongozi wabunifu wa kutatua matatizo ya eneo husika na sio wababaishaji wanaotegemea kushinda kwa rushwa.
” ,Kiongozi Upiganie haki za wanyonge ,sasa kama huna uwezo wa kutatua kero sio mbunifu kwenye bus hili la dkt.Magufuli utupishe”alifafanua Jumaa.
Awe mwadilifu na kuchukia rushwa na kupiga vita ufisadi ,atambue fursa zilizopo katika maeneo anayogombea ikiwa ni pamoja na ardhi,raslimali watu ,majengo miundombinu ili kujiinua kiuchumi ,Mpambanaji wa kutetea raslimali za umma na kusimamia mapato na matumizi .
Aidha Jumaa alieleza ,licha ya hayo CCM mkoani Pwani inajisikia faraja kuendelea kuongozwa na Rais Magufuli kwani ametekeleza mengi kimkoa ikiwemo mradi wa reli ya kisasa SGR ni Mradi unakwenda kufungua fursa za kiuchumi kwani umepita ndani ya Mkoa huo kwa asilimia 60.
“Hatua hiyo imepelekea Mkoa Pwani na kufaida kwa kujengwa kwa vituo vidogo vya abiria Substation 3 ambazo ni Soga,Ruvu,na Kwara vituo hivi kiukweli ni miji mipya ya kizazi Chetu :”
“Inakwenda kupandisha thamani ya ardhi hiyo,hii inaanisha Ardhi hii haitauzwa na kutumiwa kiholela bila ya kupimwa na kupangwa matumizi yake” alielezea Jumaa.
“Faida nyingine ni gati la Nyamisati 14BL,meli ya Mafia 5BL,SGR Zaidi ya 3TRI,Stigler ‘s -Stigo 5TR,vituo vya Afya 2BL,Maji Kisarawe zaidi ya 10 Bl,Barabara ya Makurunge – Pangani zaidi ya 250BL,Ukarabari wa Shule kongwe 1.5 BL,Umeme Vijijini serikali imetumia Bilioni 138 katika Mkoa wetu fedha ambayo imewezesha Vijiji 253 kupata Umeme;”
“Ikumbukwe kuwa Mkoa Pwani una vijiji 421 na tokea Uhuru Vijiji vilivyo na Umeme vilikuwa ni 79 tu,..”