Katibu Mkuu mstaafu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion jijini Dodoma
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo pamoja na mabalozi mbalimbali na wasanii wa TOT wakitumbuiza
……………………………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kwa kauli moja wamepitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu inayoeleza mambo yatakayotekelezwa na viongozi watakaochaguliwa kuongoza kwa miaka mitano ijayo (2020-2025).
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na wajumbe wa mkutano huo kwa kauli moja na kupitisha Ilani ya Uchaguzi Mkuu inayoeleza mambo yatakayotekelezwa na viongozi watakaochaguliwa kuongoza kwa miaka mitano ijayo (2020-2025).
Aidha katika mkutano huo Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amesema kuwa hakuna ubishi kwamba tokea umechukua nchi mambo yanakwenda vizuri, maendeleo tunayaona na uchumi umekua pamoja na mambo mengine mengi uliyoyafanya, tunakuomba uendelee vizuri hivihivi spidi isipungue”-Waziri Mkuu Mstaafu 2005-2008.
“Niwaombe wana CCM mtakapopiga kura pigeni zote kwa Magufuli bila ya kuharibu ili tumpe faraja. Kuelekea uchaguzi mkuu Niwaombe tufanye kazi kwa ushirikiano, bidii na tukatafute kura za Magufuli. Hakuna uchaguzi mwepesi. Sina mashaka hata kidogo, Magufuli atapata kura nyingi kuliko zile za mwaka 2015, pia tutapata wabunge wengi pamoja na madiwani. Tuzike tofauti zetu na tukiweke chama mbele kuliko maslahi yetu.” Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
“Kwa niaba ya vyama vya upinzani nitoe ombi kwa Chama Cha Mapinduzi, tunaingia katika uwanja wa kufanya kampeni, tushindane kwa hoja na kuwapa fursa Watanzania kuchagua viongozi wanaowataka na sisi tunakuja na ajenda, furaha kwa Watanzania inawezekana,” ametoa rai Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba
Lakini pia naye aliyekuwa Mbunge wa Momba kwa Tiketi ya CHADEMA kwa sasa ameamia CCM, David Silinde amesema kuwa amelirishwa kwa asilimia 100 kwa namna chama hiki kilivyo sasa, kuna uthubutu na namna ya kuchukua maamuzi na utekelezaji wa mambo mliyowaahidi watanzania, mambo mengi yamefanywa, tunasema asante.
Huku Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Agustino Mrema amesweka wazimkuwa Mei 4, mwaka huu sisi TLP walikaa kujadili nani awaongoze kwenye uchaguzi mkuu, Halmashauri Kuu ikasema hawana mbadala wa Rais Magufuli, ndo wakasema JPM anatosha, t tena Mei 08, kura zote zikamuangukia Rais Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama Cha TLP Augustino Mrema, na Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba ni miongoni mwa vyama vya upinzani waliohudhuria katika mkutano Mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi unaofanyika leo Julai 11, jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya ndani ya mkutano huo mbali na Mrema na Lipumba kuhudhuria pia wapo viongozi wengine wengi kutoka vyama vya upinzani waliohudhuria Mkutano huo ambao ni wakumpitisha mgombea urais Tanzania Bara kupitia Chama cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi waJakaya Kikwete ambapo ni makao makuu ya CCM Dodoma.