DKT.MAGUFULI KUGOMBEA URAIS TANZANIA KUPITIA CCM

0

 

…………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wamempitisha Ndugu John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kwa kura 1822 ambayo ndio idadi ya wajumbe waliohudhuria na ni asilimia 100 ya kura zote.

Akitangaza matokeo hayo aliyekuwa Spika wa bunge Job Ndugai katika mkutano Mkuu uliofanyika leo jijini Dodoma.

Aidha Dkt.Magufuli ndo amepewa dhamana ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 Tanzania bara huku Zanzibar ni Dkt.Hussein Mwinyi.