********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wananchi wametakiwa kufika kwenye banda la Mamlaka ya MApato TAnzania (TRA) kwenye Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere kwaajili ya kupata elimu kuhusu ulipaji kodi pamoja nakupata huduma nyingine zinazohusu Mamlaka hiyo kwa wepesi zaidi.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani (TRA) Bi.Tubagile Namwenje baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 44 ya biashara Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika banda hilo Bi.Tubagile amesema kuwa lengo la kuwepo kwa banda hilo ni kutoa elimu kwa wananchi na wawe na ufahamu wa kodi.
“Mchango wetu ni kwamba tusaidie nchi kuweza kujitegemea ikiwa kila mwananchi atafanya kazi kwa nguvu zake zote na weledi wake wote na kulipa kodi kwa uwaminifu kweli tutafurahi kuwa kwenye uchumi wa kati na ni kitu ambacho kila mtu anakitaka hakuna mtu ambaye anapenda kuwa ombaomba”. Amesema Bi.Tubagile.
Kwa upande wake Mchumi-TRA, Bw.Aulelus Myamba amesema kuwa mamlaka hiyo imeweza kurahisisha uondoshaji wa mizigo bandarini tofauti na zamani.
“Mwanzo ulikuwa ni mgumu ila kwasasa unaweza kuondosha kontena la mizigo bandarini pale ndani ya siku 7, zamani tulikuwa tunaweza kutumia siku 30 kuondosha mzigo , hicho kimeweza kusadia wafanyabiashara kwenda kufanyabiashara zao kwa urahisi zaidi na kwa haraka kuweza kutengeneza faida na kuweza kujenga uchumi wa nchi”.Amesema Bw.Myamba.
Aidha Bw.Myamba amesema TRA imeweza kudhibiti biashara za magendo mipakani hii imeweza kusaidia kurahisisha au kuwezesha biashara kuwa shindani baina ya wafanyabiashara kuliko zamani.
Nae mfanyabiashara ambaye amefika katika banda la mamlaka hiyo Bw.Laurent Paul amesema huduma zinazotolewa na TRA katika viwanja vya Maonesho zinaridhisha kwa kaisi kikubwa kwani kila mteja afikapo kwenye banda hilo anahudumiwa ipasavyo.
“Ukweli ni kwamba huduma zinazotolewa na TRA hapa Sabasaba zinaridhisha kwa kiasi kikubwa, naona wenzangu wengi wanakuja na kuhudumiwa wanatabasamu inaonesha kuwa ninamna gani huduma nzuri zinatolewa”. Amesema Bw.Paul.