Home Siasa DKT. MWINYI KUPEPERUSHA BENDERA YA  URAIS CCM ZANZIBAR

DKT. MWINYI KUPEPERUSHA BENDERA YA  URAIS CCM ZANZIBAR

0

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM kimempitisha Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Uraisi Zanzibar kupitia CCM.

Dk.Mwinyi amepata  kura 129 sawa na asilimia 78.65, Nafasi ya pili imeshikwa na  Dk Khalid Salum aliyepata kura 19 sawa na asilimia 11.58 huku Nafasi ya tatu ikishikwa na Shamsi Vuai Nahodha aliyepata  kura 16 ambazo ni sawa na asilimia 9.75 .

Sasa ni rasmi Dk.Mwinyi atapeperusha bendera ya CCM Zanzibar katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.