Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Mikoa wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akiongoza kikao na majadiliano kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe .Martine Shigela,akichagia mada kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kilichofanyika leo jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.. Anna E. Mghwira akichagia mada katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab R. Telack,akisisitiza jambo wakati akichagia mada katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi,akichagia mada katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kilichofanyika leo jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau Kilimo cha Mkonge nchini wametakiwa kuhamasisha wananchi kufanya kilimo cha kibiashara na kuhacha kufanya kilimo cha kujikimu ili kuinua kipato chao na kukuza uchumi wa taifa.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba leo Jijini Dodoma katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa ambao ni wadau wa kilomo cha zao la Mkonge juu ya kuangalia mikakati ya kufufua na kuboresha kilimo cha zao la Mkonge Nchini.
Aidha Mhe. Mgumba amesema kuwa serikali imejipanga kurudisha hadhi ya zao la mkonge nchini hivyo ni wakati sahihi wa kuweka mikakati Madhubuti ya kuhamasisha watanzania kulima zao la mkonge kwa kufanya zao hilo kuwa la kibiashara ili kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja .
“Kilimo cha kulima kwaajiri ya kujikimu kimepitwa na wakati kwa sasa kilimo sahihi ni kilimo cha kibiashara kitakacho wasaidia watanzania na taifa kwa ujumla kwa kuongeza pato la taifa kwa kuuza mazao yetu ndani nan je ya nchi”amesisitiza Mhe. Mgumba.
Kwa upande wa wizara ya kilimo wao wameandaa mikakati Madhubuti ya kutekeleza ili kuhakikisha zao la mkonge linafanyikiwa kwa kiasi kikubwa nchini na kuleta tija kwa watanzania.
Katika kikao hicho kila mkuu wa mkoa alipata kutoa taarfa juu ya zao la mkonge katika mkoa wake ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameweka wazi kuwa katika zao hilo watanzania wasitegeme watu wa kigeni kuja kulifufua zaidi watanzania wao kuchukua hatua ya kutumia zao hilo kwa manufaaa ya wakulipa na taifa kwa ujumla.
Pia Bi Telack ameshauri kuwa sasa ni wakati sahihi wa wataaalamu wa kilimo kuwasaidia wakulima juu ya kuona namna ya kuzalisha zao hilo kwa wingi ili kufikia malengo makubwa ya taifa katika zao la mkonge.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa akitoa wito kwa wizara ya kilimo kuanzisha chuo cha utafiti juu ya kujua thamani ya mazao ya kilimo inchini ili kuwa muongozo bora kwa wataalamu wa kilimo na wakulima kwa ujumla.