Mhandisi Mtafiti TANESCO Aurea Bigirwamungu (kwanza kulia) akiwa na watumishi wa TANESCO katika Kiwanda cha Mchele na Alizeti wilayani Dodoma.
Muonekano wa Baadhi ya mitambo katika Kiwanda cha Nyanza Road Workers kilichopo wilayan Bahi.
Mhandisi Mtafiti Aurea Bigirwamungu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kiwanda cha Nyanza Road Workers wilayani Bahi baada ya kutoa mafunzo ya Elimu juu ya Matumizi bora ya Nishati ya Umeme
……………………………………………………………………
Na.Alex Sonna, Dodoma
Wamiliki wa Viwanda Wilaya za Dodoma na Bahi watakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya ukarabati wa mara kwa mara na kubadili vifaa vilivyo tumika kwa muda mrefu ili kuepuka gharama zisizo za lazima na matumizi makubwa ya nishati ya umeme.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mhandisi Mtafiti wa TANESCO, Aurea Bigirwamungu wakati wa kutoa elimu juu ya matumizi bora ya Nishati ya Umeme katika wilaya za Dodoma na Bahi.
Aidha Bigirwamungu ameshauri wamiliki hao kuwa na utamaduni wa kubadilisha moto za kuendeshea mitambo yao katika uzalishaji ili kutumia nishati ya umeme inayoendana na gharama ya matumizi sahihi ya nishati ya umeme katika viwanda vyao.
Naye Afisa Tawala wa Kampuni ya Nyanza Road Workers, Bakari Mugini amesema kuwa mafunzo hayo wamefahidika kwa kujua matumizi vyema ya umeme ili kuendana na matumizi sahihi ya nishati ya umeme katika kampuni hiyo.
Mugini ameeleza kuwa katika mafunzo hayo wamepata elimu juu ya usalama wa miundombinu iliyopo katika viwanda ili kuongeza uzalishaji katika shughuli za kampuni zao.
“Kipekee nalipongeza shirika la TANESCO kwa utendaji bora juu ya kusambaza nishati ya umeme na kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha umeme Mkoani Dodoma unakuwa wakutosha na unapatikana bila matatizo na kama kna tatizo basi wananchi mnataarfiwa awali na baada ya marekebisho ya kiufundi umeme unarejea na shughuli zinaendelea “, ametoa pongezi Mugini.