Home Biashara TBL Plc kuendelea kuunga mkono kampeni za usalama barabarani

TBL Plc kuendelea kuunga mkono kampeni za usalama barabarani

0

Meneja Mawasiliano wa TBL Plc ,Amanda Walter (wa pili kulia) akikabidhi  T-Shirt za uhamasishaji kampeni za Usalama barabarani zilizotolewana kampuni  kwa Kamishna Msaidizi  wa Polisi kutoka kikosi cha usalama barabarani, ACP Mkadam Mkadam katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam ,wengine pichani ni Maofisa wa jeshi la polisi Kikosi cha Usalama barabarani.

Meneja Mawasiliano wa TBL Plc ,Amanda Walter (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ACP Mkadam Mkadam (wa pili kutoka kushoto) na askari wa kikosi cha usalama barabarani wakati wa hafla hiyo.

**************************** 

Kampuni ya bia ya TBL Plc, imeeleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kufanikisha kampeni za Usalama barabarani nchini kwa ajili ya kupunguza matukio ya ajali nchini.

Meneja Mawasiliano wa TBL Plc, Amanda Walter, aliyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi  T-shirts za uhamasishaji wa kampeni za usalama barabarani zilizotolewa na kampuni kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani.

Alisema T-Shirts hizo zina jumbe mbalimbali za kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari dhidi ya janga baadhi ya jumbe zikiwa Tii sheria , Zuia ajali,Okoa maisha , Kamata usukani wa Maisha yako na Kunywa kiustarabu .

Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo Kamishna Msaidizi  wa Polisi kutoka kikosi cha usalama barabarani, ACP Mkadam Mkadam,alishukuru TBLPlc kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kampeni za kutokomeza ajali na kuwataka wadau wote na jamii nzima kwa ujumla kushirikiana na Serikali ili kupunguza matukio ya ajali nchini ambazo zimekuwa zikigharimu maisha na kuleta hasara.