Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akipewa maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Karatasi cha Mgololo, Gregory Chogo wakati alipotembelea jana Kiwanda cha Kuzalisha Karatasi Mgololo ( MPM) kwa lengo la kujua changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanapohitaji Malighafi kutoka katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi katika mkoa wa Iringa. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mufindi, Endrew Musimbwa.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mufindi pamoja na Watumishi wa Shamba la Miti Sao Hill akizungumza na Mwekezaji wa Kiwanda cha Kuzalisha Karatasi Mgololo, Kashamiri, Shamir ( wa tatu kushoto) mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuzungumza na Wanunuzi wakubwa wa Malighafi kutoka katika Shamba la Miti la Sao Hill.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameshika karatasi zinazozalisha katika Kiwanda cha Kuzalusha Karatadi Mgololo akipewa maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Karatasi cha Mgololo, Gregory Chogo wakati alipotembelea jana katika kiwanda hicho kujionea uzalishaji.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amekutana na kufanya mazungumzo Wanunuzi Wakubwa wenye viwanda wanaonunua malighafi inayozalishwa kutoka katika Shamba la Miti Sao Hill lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.