Home Biashara MATUKIO MBALIMBALI YA WAGENI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

MATUKIO MBALIMBALI YA WAGENI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, SACP Chacha Bima, akioneshwa moja ya machapisho ya Huduma Ndogo za Fedha lenye kanuni zinazohusika katika kujisajili na Kamishna Msaidizi Idara ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dioninsia Mjema, kushoto ni Afisa Usimamizi wa Fedha Bi. Limi Bulugu, wakati wa maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara yanayoendelea katika Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHANA) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Stella Kyamba, akimwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, SACP Chacha Bima, jinsi ya kujisajili ili kupata huduma ya hati ya mshahara kwa njia ya mtandao, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara yanayoendelea katika Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Jijini Dar es Salaam. 

Mchumi, Bw. Eliudi Yesaya, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, akiowaonesha wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam, moja ya machapisho yaa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo  pamoja na Taasisi zake wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha na Mipango)