Home Michezo MASHINDANO YA GOLF YA UJIRANI MWEMA YAMALIZIKA MOROGORO

MASHINDANO YA GOLF YA UJIRANI MWEMA YAMALIZIKA MOROGORO

0
*************************
Mashindano ya ujirani mwema ya Golf kati ya timu ya dar bogey, break fast na baadhi ya wachezaji wa MM kutoka Lugalo yaliyofanyika kwa siku mbili mkoani Morogoro yamemalizika.
Akizungumza baada ya Mchezo Mpiga Mikwaju Kiki Ayonga kutoka Dar bogey aliyepata net ya 67 ameelezea kuhusu ushindi wake kwa siku ya pili ya mashindano hayo ambayo katika siku ya kwanza Mchezaji wa Kualikwa Nicholous Chitanda aliibuka na Ushindi.

kwa upande wa wachezaji wanawake waliokuwa katika msafara huo Josephine Njoroge na Maryanna Mugo wameelezea changamoto walizokutana nazo katika uwanja wa morogoro.

Naye Katibu wa golf morogoro Anitha Siwale amewapongeza wachezaji wa Lugalo Golf kwa kutembelea Morogoro.