******************************
Arusha, 1 Julai 2020
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inapenda kuufahamisha Umma kuwa, katika ukaguzi wake wa kawaida wa kisheria kama ilivyotolewa katika ripoti ya Julai 1, 2020, TAEC imesimamisha utoaji wa huduma ya mionzi katika vituo 95 kwa kutokidhi matakwa na vigezo vya usalama wa mionzi kama ilivyoainishwa katika Sheria Namba 7 ya Nguvu za Atomiki ya Mwaka 2003 ikisomwa pamoja na kanuni zake.
Matakwa na vigezo hivyyo vya kisheria vilivyokiukwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wenye sifa katika kutoa huduma za mionzi, majengo yasiyokidhi vigezo na viwango vilivyowekwa kisheria, ubovu wa mashine wa mashine zinazotoa mionzi na utoaji wa huduma hiyo bila kuwa na leseni kinyume na Sheria tajwa hapo juu.
Kwa upande wa huduma za uchunguzi wa kitabibu vituo vilivyofungiwa ni pamoja na; Kituo cha Afya cha Kaloleni, Kituo cha Afya cha Kansay, Hospitali ya Wilaya ya Karatu, Hospitali ya Wilaya ya Meru, Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, Kituo cha Afya cha Mong’ola (Arusha), Al-Hilal Polyclinic, Hospitali ya Mnazi Mmoja (Idara ya Meno), Hospitali ya Mwananyamala (Idara ya Meno), Hospitali ya Sanitas, Hospital ya Sino Tanzania Friendship, Kituo cha Afya cha Arafa Majumba Sita (M6), Kituo cha Matibabu cha Mselemu, Kituo cha Afya cha Magomeni (Idara ya Meno), Kituo cha Afya cha Magereza – Ukonga, Kituo cha Afya cha Mama Ngoma, Kituo cha Afya cha Sinza (Idara ya Meno), Hospitali ya St Bernard, Kituo cha Afya Dar es Salaam, Kituo cha afya cha Al-Jumaa, Kituo cha Afya cha Kigamboni, Kituo cha Afya Salaamani Tandika (Dar es Salaam), Mlali Rehabilitation Centre, Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, Hospitali ya Mirembe (Dodoma), Hospitali ya Mugana, Hospitali ya Mtakatifu Joseph Kagondo, Hospitali ya Nyakaiga, Hospitali Teule ya Rubya, Hospitali ya Ufufuo, Kituo cha Afya cha Nyamiaga (Kagera), Hospitali ya Wilaya ya Gonja, Kituo cha Afya cha Alfa na Omega, Kituo cha Afya Bwambo, Kituo cha Afya cha Kilimanjaro, Kituo cha Afya cha Mtakatifu Joseph Uchira, Kituo cha Afya cha Papri, Kituo cha Matibabu ya Saratani ya Ngozi – Moshi (Kilimanjaro), Hospitali ya Misheni ya Kipatimu, Hopitali ya Wilaya ya Kinyonga (Kilwa Kivinje), Hospitali ya Rondo (Lindi), Hospitali ya Kiluteli ya Ilula Hospitali (Iringa), Hospitali ya Wilaya ya Babati, Kituo cha Afya cha Balang’dalalu, Kituo cha Afya cha Gendabi (Manyara), Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Hospitali ya Misheni ya Kibara (Mara), Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Hospitali ya Kiluteri ya Matema (Mbeya), Hospitali ya Dilsan, Hospitali ya Wilaya ya Mahenge, Kituo cha Afya cha Shalom, Hospitali ya Mtibwa, Kituo cha Afya cha St. Harry (Morogoro), Hospital ya Wilaya ya Ukerewe, Hospitali ya Wilaya ya Misungwi (Mwanza), Hospitali ya Bulongwa, Hospitali ya Uwemba (Njombe), Hospitali ya Wilaya ya Utete (Pwani), Hospitali ya Dr. Atiman, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Sumbawanga, Hospitali Teule ya Wilaya Namanyere, Kituo cha Afya cha Mvimwa, Kituo cha Afya Nkomolo (Rukwa), Hospitali ya St. Elizabeth – Lituhi (Ruvuma), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Shinyanga, Kituo cha Afya cha Igalilimi (Shinyanga), Hospitali ya Wilaya ya Meatu, Kituo cha Afya cha Maganzo (Simiyu), Hospitali ya Iambi Singida, Hospitali ya Wilaya Kiomboi, Hospitali ya Wilaya ya Manyoni (Singida), Kituo cha Uchunguzi cha Jema, Kituo cha Afya cha Tumaini EAGT (Songwe), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete (Tabora), Hospital ya Mtakatifu Francis kwa Mkono, Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Hospitali ya Wilaya ya Pangani, (Tanga).
Kwa upande wa ukaguzi wa mizigo vituo na ujenzi wa barabara vilivyofungiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato – Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Mutukula – Kagera, Uwanja wa Ndege wa Bukoba Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Mwanza, Skol Building Contractor – Sinza Africa Sana, TANROAD – Dar es Salaam, TANROAD – Dodoma, TANROAD – Kagera, TANROAD – Mwanza, TANROAD – Shinyanga, TANROAD – Tanga.
Kusimamishwa kwa vituo hivi ni kutokana na ukaguzi unaoendelea kufanywa kila mahali nchini ili kuhakikisha uzingatiaji wa sheria za usalama za mionzi kama ilivyoainishwa katika Sheria na kanuni zake zinazohusika ili kulinda wafanyakazi, wagonjwa, wananchi na mazingira dhidi ya athari mbaya za mionzi.
TAEC inahimiza Vituo vyote vinavyotoa / kutumia huduma za mionzi kuhakikisha vinafuata masharti na kanuni za usalama wa mionzi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Nguvu ya Atomiki Namba 7 ya mwaka 2003 pamoja na kushirikisha wataalamu wa TAEC katika hatua zote za utoaji wa huduma ya mionzi kuanzia ujenzi wa vituo vyao kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kisheria.