Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Sango Songoma akiongea na jumuiya ya Shule ya Sekondari ya Lulumba (hawaonekani pichani) baada ya kukabidhiwa miundombinu na vitakasa mikono kwa ajili ya matumizi ya shule. Lulumba ni moja ya shule iliyofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kitaifa hapa nchini.
Picha ya pamoja kati ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lulumba, Uongozi wa Wilaya ya Iramba na Wataalam wa Wizara ya Maji baada ya hafla fupi ya kuikabidhi shule hiyo vifaa na miundombinu ya kunawa mikono shuleni hapo wilayani Iramba, Kwa niaba ya Katibu Mkuu – Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Maji Mhandisi Lyidia Joseph (kushoto), akikabidhi kitasamkono, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwalimu Lino Mwageni, ikiwa ni sehemu ya msaada wa miundombinu ya kunawa mikono na vitakasamikono kutoka Wizara ya Maji katika jitihada za kutunza afya za wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lulumba.
Picha ya pamoja baina ya Wataalam wa Wizara ya Maji, na Walimu wa Shule ya Seondari ya Lulumba baada ya kukabidhiwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya COVID 19, pia kuimarisha usafi wa wanafunzi wakati wote baada ya shule kufunguliwa.