Home Michezo MCHEZAJI NICHOLOUS CHITANDA WA LUGAOLO AMEIBUKA MSHINDI WA SHINDANO DOGO LA UJIRANI...

MCHEZAJI NICHOLOUS CHITANDA WA LUGAOLO AMEIBUKA MSHINDI WA SHINDANO DOGO LA UJIRANI MWEMA KATI YA LUGALO NA MOROGORO.

0

*********************************

AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA MASHINDANO HAYO YALIYOANDALIWA NA KIKUNDI CHA GOLF KUTOKA LUGALO CHA DAR BOGEY CHITANDA AMEAHIDI NA KESHO KUFANYA VIZURI.
KWA UPANDE WAKE NAHODHA WA DAR BOGEY GEORGE KIVARIA AMESEMA HUU NI MWANZO NA WANA MPANGO WA KUZUNGUKA VILABU VINGINE BAADA YA WIKI HII KUWA MOROGORO.
NAYE MAKAMU MWENYEKITI WA KLABU YA GOLF  MWENYEJI YA MOROGORO  LOUIS ROUSSOS AMESEMA UJIO WA WACHEZAJI HAO NI FARAJA KWA KLABU HIYO.
MASHINDANO HAYO NI YA SIKU MBILI NA YANATARAJIWA KUMALIZIKA KESHO JUMAPILI NA WACHEZAJI KUREJEA JIJINI DAR ES SALAAM.