Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu jana akiwa ameongoza na Watumishi wa Shamba laMiti la Sao Hill akipewa maelezo na Afisa Misitu, Glory Fortunatus wakati alipokuwa akitembelea bustani ya miti ya shamva hilo lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na Askari Wahifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mara alipowasili katika makao makuu ya wilaya ya Mufindi kwa ajili ya ziaracya kikazi ya siku moja katika Shamba la Miti la Sao Hill lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Shamba la Miti la Sao Hill wakati alipofanya ziara ya kutembelea bustani ya miti katika shamba hilo lilipo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongoza na baadhi ya Watumishi wa Shamba la Miti Sao Hill wakati akikagua vifaa maaalum vya kuoteshea miti kabla ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa.Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe.Constantine Kanyasu akizunguma na Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill pamoja na Afisa Misitu Glory Fortunatus ( wa kwa kushoto) wakati akiangalia miti iliyooteshwa kwa vifaa maalumu ambayo ipo tayari kwa ajili ya kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa.
( Picha zote na Wizara ya Malasili na Utalii)
************************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Constantine Kanyasu ameonesha kusikitishwa na uwepo wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 baina ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) ambazo zote ni Taasisi za Serikali kuwa jambo hilo sio la kawaida.
Ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Shamba la Miti la Sao Hill linalosimamiwa na TFS lililopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Amesema eneo hilo la ardhi lenye mgogoro lina ukubwa wa hekta 1705 ambazo kati ya hizo hekta 600 zilishapandwa miti na TFS ila baada ya mgogoro huo kuibuka kila Taasisi ikidai kuwa eneo hilo ni lake ilipelekea TFS kushindwa kumalizia kupanda miti katika eneo lililokuwa limebaki lenye jumla ya hekta 800.
Kufuatia hali hiyo, Mhe. Kanyasu ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ishughulikie mgogoro huo uliopo baina ya JKT Mafinga na Shamba la Miti Sao Hill ili kila Taasisi ijikite kwenye majukumu yake ya msingi.
” Mgogoro huu usipotafutiwa ufumbuzi wa haraka utaleta athari, Kitendo cha JKT Mafinga kung’oa vigingi vilivyowekwa na TFS kwa ajili ya kubainisha mipaka haileti picha nzuri ikizingatiwa kuwa zote hizo ni Taasisi za Serikali” alisisitiza.
Amesema endapo Kamati hiyo Ulinzi na Usalama itafika mwisho na kushindwa kupata majibu juu ya mgogoro huo imshirikishe Mkuu wa mkoa wa Iringa ili mgogoro huo uweze kuisha.
Amesema ni lazima mgogoro huo ufike mwisho na ikishindikana Mkuu wa Mkoa ashirikishwe hali itakayosaidia kuleta suluhu ya kudumu na kuzifanya Taasisi hizo kuendelea kutoa huduma kwa jamii badala ya kuendelea kusigana kila kukicha.
” Nina amini Mkuu wa mkoa ana vyombo na. uwezo wa kumaliza mgogoro huu kwa vile hizi zote ni Taasisi za Serikali” alisisitiza Mhe.Kanyasu
Hata hivyo, Mhe.Kanyasu amesema endapo Mkuu wa Mkoa atashindwa kuutafutia majibu mgogoro huo basi aitaarifu Wizara ya Maliasili na Utalii ili iweze kukutana Wizara husika kwa lengo la kumaliza mgogoro huo.
Amesema anataka mgogoro huo ufike mwisho na kama nyaraka zitaonesha kuwa eneo hilo la JKT basi JKT wapewe na kama ikithibitika ni eneo hilo ni mali ya TFS wapewe ili waweze kupanda miti.
” Jukumu letu sisi ni kupanda miti tunachotaka ni kuona eneo hilo linapandwa miti bila kujali kapanda nani JKT au TFS ” alisisitiza Mhe.Kanyasu.
Hata hivyo, Mhe.Kanyasu amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuushughulikia mgogoro huo licha ya kuwa umekuwa ukienda taratibu sana na hivyo kasi ya TFS kumalizia kupanda miti katika eneo hilo imekuwa ikitatizwa na kuwepo kwa mgogoro huo.
Kwa upande wake, Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Juma Mwita amesema mgogoro huo wa ardhi