Mnamo tarehe 27 Juni mwaka huu Tecno Mobile Tanzania kwa kushirikiana na Startimes Tanzania ilitembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Chanika hapa hapa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa misaada mbalimbali ikiambata na elimu ya masuala ya kiafya ambapo pia watapata vifaa vya kujikinga na virusi vya homa ya mapafu (covid-19) pamoja na ushauri wa ujasiriamali.
Tecno Mobile Tanzania imedhamiria kuwasaidia na kuwaelimisha watoto hao juu ya masuala mbalimbali ya kifedha, ujasiriamali na elimu ya afya juu ya kujikinga na homa ya mapafu (covid-19) na kwa kuhakikisha hayo yanakwenda vizuri tulikua na mtaalamu wa saikolojia hapa nchini MC Anthony Luvanda pamoja na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Her Initiative’.
Pia sisi kama Tecno Mobile Tanzania tumedhamiria kutoa misaada mbalimbali kama tulivyoainisha awali lakini hatutoishia kwa watoto pekee kwa sababu tunatambua uwepo wa wafanyakazi wa kituo husika ambao watapata pia vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya homa ya mapafu (covid-19)
Washirika wetu Startimes Tanzania wamedhamiria kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapa kingamuzi kipya chenye kifurushi cha mwaka mzima kitakachoonyesha channel zinazotoa mafundisho kwa ajili ya watoto. Shirika tajwa hapo juu lisilo la kiserikali linategemea kuwaacha watoto hawa na elimu ya afya nzuri, kujitambua pamoja na ujasiriamali.
Kwa kumalizia tungependa sana kuwashukuru washirika wetu wote waliokubali kushirikiana nasi katika siku hii muhimu sana kwa kampuni yetu inayojali jamii yetu pendwa inayotuzunguka.