Home Mchanganyiko ELIMU YA FISTULA YA UZAZI PASUA KWA KICHWA KWA JAMII

ELIMU YA FISTULA YA UZAZI PASUA KWA KICHWA KWA JAMII

0

Mratibu wa Shirika la MAPERECE, Lavits John Bifandimu, akito mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo Mabalozi wa Fistula ya Uzazi wilayani Nyamagana.

Mabalozi wa Fistula ya Uzazi kutoka katika Kata 18 za Wilaya ya Nyamagana wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo yalitolewa na Shirika la MAPERECE la wilayani Magu.
Picha na Baltazar Mashaka  
*********************************
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
UELEWA mdogo wa jamii kuhusu ugonjwa wa fistula ya uzazi  visababishi vyake na matibabu yake  unaathiri mtitiriko wa wanawake wengi wenye matatizo hayo  kwenda kutibiwa.

 

Hayo yalielezwa jana jijini Mwanza na Daktari Kiongozi wa Wodi ya Magonjwa ya Vizazi na Uzazi wa Hospitai ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) Dk. Reolvin Elishaphat, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mabalozi wa Fistula Wilaya ya Nyamagana.

 

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la Kutetea Haki za Wazee, Wanawake na Watoto la Magu Poverty Focus on Older People Rehabilitation Centre (MAPERECE) yakilenga kuwaibua wagonjwa wapya wa fistula na kuwapeleka kwenye matibabu.

 

Dk. Elishaphath alisema  uelewa  wa jamii juu ya ugonjwa wa fistula na wapi matibabu yake yanapatikana uko chini hali inayosababisha wanawake wanaogua ugonjwa huo kujenga dhana kuwa wamelogwa, ugonjwa unao waathiri wanawake wenye kipato kidogo wanaojifungulia kwa waganga wa jadi.

 

“Ututakuta wahanga watano, watatu hawajui kusoma wala kuandika, inaonyesha uelewa wa jamii uko chini kuhusu huduma za afya ya uzazi.Hivyo mafunzo haya tunataka watu waelewe tatizo la fistula,chanzo chake, dalili, madhara na matibabu yake, dalili, madhara ili kuondoa dhana ya kulogwa ama  unasababishwa kujamiiana na wanaume wengi,”alisema.

 

Kiongozi huyo wa wodi ya magonjwa ya vizazi na uzazi alisema ugonjwa wa fistula unatibika ambapo mafunzo yanayotolewa kwa mabalozi wa fistula yatawasaidia kutoa rufaa na usafiri kwa wagonjwa  kwenda kwenye hospitali zinazotoa huduma ya tiba ya fistula.

 

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, mwaka 2015 wanawake 1,337 walijitokeza kutibiwa fistula , 2016 waliopata tiba ni 1,356 ambapo 2017 idadi ilishuka na  wanawake 1,060, mwaka walitibiwa 900 na mwaka jana waliopata tiba walikuwa 852.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MAPERECE, Julius Mwongela alisema tatizo la ugonjwa wa fistula ya uzazi ni kubwa kwenye jamii hasa vijijini kutokana na changamoto mbalimbali za ukosefu wa elimu, uchumi na huduma duni za afya ya uzazi zinazotolewa.

 

Alisema wahanga wakubwa na walio kwenye hatari ya kupata fistula ni wasichana wa umri chini ya miaka 18 kutokana na kupata mimba za utotoni ambapo nyonga zao zinakuwa hazijakomaa na hivyo kupata majeraha makubwa kulinganisha na wenye umri wa zazidi ya miaka 18.

 

“Hapa tunapiga debe kuishawishi serikali kulibeba suala la fistula liingizwe kwenye Afya ya Mama na Mtoto kwa sababu  wanawake wenye tatizo hilo wametengwa wakati yote yanahusu uzazi.Wizara ikilichukua watatambuliwa na kutibiwa bure vinginevyo itakuwa ni kuwabeza wanawake wenye fistula,”alisema Mwongela.

 

Aidha alidai kuwa changamoto ya kuwabaini wagonjwa wa fistula ni kikwazo kwani wengi wanaopata tatizo hilo hufanya siri ama wanakuwa wmeathirika kiakili na kisaikolojia na hivyo kutojiweka wazi.

 

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Juma Mfanga, Mratibu wa Afya ya Uzazi Wilaya ya Nyamagana, Bertha Yohana aliwataka mabalozi hao wa fistula elimu hiyo waitumie kuleta mabadiliko chanya kwenye na kuibua wagonjwa wapya