Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama Bw. Anderson Msumba akitoa ufanunuzi kwa kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga kuhusu eneo lilotengwa kwa ajili ya uwekezaji viwanda nje kidogo ya kiwanda kinachojengwa na mwekezaji mzawa anayewekeza katika kiwanda cha maji na vifungushio kwenye eneo la Nyashimbi nje kidogo ya Mji wa Kahama.
Menyekiti wa Kamati wa Kamati ya Amani ya Mkoa Shekhe Balilusa Khamisi akifafanua jambo wakati wa ziara ya kamati yake Wilayani Kahama kujionea Miradi ya Afya na Uwekezaji Wilayani humo kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Anamlingi Macha.
Wajumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga wakiangali mashine inayojengwa kwa ajili kusaga mawe ya kuchenjulia madini kutoka katika kalakana ya mwekezaji mdogo iliyoko eneo la Bukonda Moyo nje kidogo ya Mji wa Kahama.
…………………………………………………………………………………….
Na mwandishi wetu ,Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Anamlingi Macha amesema Mkakati wa miaka mitano ambao dira yake ni kutoa uduma bora katika Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa maendeleo aendelevu katika Halmashauri ya Mji Kahama imeendelea kutoa huduma bora za kiuchumi,kijamii na kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Bw. Macha amesema hayo jana alipokutana na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyamnga iliyotembelea Wilaya yake kujionea miradi ya Afya na uwekezaji inayoendelea na iliyokamilika katika Wilaya Kahama na Wilaya nyingine za Mkoa wa Shinyanga.
Bw. Macha akiongea mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo aliongeza kuwa mpango mkakati huo utekelezaji wake umezingatia matarajio ya Serikali yaliyoainishwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Malengio endelevu ya Milenia ikiwemo miongozo ya Kisekta pamoja na Mpango wa maendeleo wa Serikali wa miaka mitano .
Aidha Bw. Ameongeza kuwa Halamashauri ya Mji Kahama imeweza kutenga maeneo kwa ajili ya uendelezaji viwanda ambayo ni kwa ajili ya uendelezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa na kuongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto za uendelezaji wa miundombinu ya barabara kuelekea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya maendeleo ya viwanda.
Akiongea kuhusu suala la Amani katika Wilaya ya Kahama Mkuu huyo Wilaya alisema kuwa Wilaya ya Kahama kwa ujumla iko salama nakutaja baadhi ya matendo yaliyowai kujitokeza kama imani za kishirikiana kwa mauaji ya watu wenye ualibino kuwa yamepungua sana na sasa Wilaya yake iko shwari.
Akiongea wakati wakati wa majumuisho Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga Shekhe Balilusa Khamisi aliitaka serikali kushirikisha viongozi wadini pale ambapo inakumbana na changamoto mbalimbali ili viongozi hao wawezi kushiriki kuyatatua kwa kuyaweka katika maombi jambo ambalo litachangia katika ustawi wa amani hapa Nchini.
Akiongea suala la ramli chonganishi na changamoto nyingine zinazojitokeza katika Jamii Shekhe Khamisi aliongeza kuwa serikali ya Mkoa imekuwa ikiwashirikisha na kwa kiasi kikubwa matendo hayo yamepungua kutokan na viongozi wa dini kualisemea kwa nguvu zote kupitia majengo ya ibada.
Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga inayoongozwa na viongozi wa dini kutoka Mkoa wa Shinyanga inaendelea na ziara ya siku tatu katika Wilaya za Mkoa wa Shinyanga kujionea baadhi ya miradi ya Afya na Uwekezaji na tayari imekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Mji Kahama .