Home Mchanganyiko MSANGUKA ATIA NIA KUGOMBEA UBUNGE MBARALI

MSANGUKA ATIA NIA KUGOMBEA UBUNGE MBARALI

0

…………………………………………………………….

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Yunus Msanguka ametia nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Mbarali.

Akizungumza na Mwandishi wa Fullshangwe blogu  Kada huyo amesema amefikia uamuzi huo ili kuweza kusukuma gurudumj la maendeleo kwa Wana Mbarali.

Amesema kuwa anachosubiri ni katika mchakato ndani ya chama akipita hapo ni kuipepelusha bendera ya chama hicho.

Amesema uwezo anao wa kupeperusha bendera hiyo kutokana na kuwa karibu na wananchi wa Jimbo hilo.

Aidha amesema kuwa kazi ni kuendeleza mazuri zaidi kutokana na sera za Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwainua wanyonge.

Msanguka amesema Mbarali ikifanikiwa kupita itabadilika Sana kutokana na michango yake katika kuweza kutatua changamoto.

“Hapa ninachosubiri ni kuungwa mkono na wanachama wa Jimbo kunichagua kwa lengo moja ya kupigania maendeleo ya wanambarali na kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kwenda kisasa zaidi kuleta mabadiliko ya kiuchumi”amesema Msanguka.

Hata hivyo amesema kama kijana amekuwa na maono mengi ya kutaka vijana kuinuka kiuchumi kutokana na mbarali kuwa na ardhi yenye rutuba kwa kwenda katika kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea.