Home Mchanganyiko HALIMASHAURI 28  ZATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI MPYA NDANI YA MIEZI MITATU

HALIMASHAURI 28  ZATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI MPYA NDANI YA MIEZI MITATU

0

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima (kulia) akiwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Chalinze, Dkt. Allen Mlekwa 

Mwonekano wa eneo lililosafishwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze leo baada ya kufanya ziara ya kustukiza mkoani Pwani.

Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima(hayupo pichani) leo katika ziara yake ya kustukiza katika wilayani humo.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima akitoa maelekezo kwa watumishi wa hospitali ya wilaya ya Chalinze leo katika ziara yake ya kustukiza mkoani Pwani.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma katika hospitali ya wilaya ya Chalinze .

…………………………………………………………………………………

Na. Majid Abdulkarim , Pwani

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima leo amefanya ziara ya kustukiza katika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali mpya ya halmashauri ya Chalinze.

Hospitali hiyo ni kati ya 28 mpya zinazojengwa katika halmashauri mbalimbali nchini ambazo, mwishoni kwa mwaka wa fedha wa 2019/20 Serikali imetoa Tsh bilioni 14 kwa wastani wa Tsh milioni 500 kila moja ili kuanza ujenzi wa majengo mbalimbali.

Dkt Gwajima ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Chalinze kwa kuanza vizuri na kutumia siku zao 14 za mandalizi ya uratibu wa ujenzi.

“Kwa sasa tayari eneo limeshasafishwa na vifaa vinapokelewa kesho kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi “Ameeleza Dkt Gwajima

Aidha Dkt. Gwajima ameelekeza majengo ya awamu hii ya kwanza yakamilike ndani ya muda usiozidi miezi miwili.

Lakini pia Dkt Gwajima , amezitaka halmashauri zote zilizopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa awamu hii kuweka ratiba ya kazi gani zitafanyika kila siku huku wataalamu wa afya wakiwa karibu na utekelezaji huo katika kila hatua na kutoa taarifa ya maendeleo kila baada ya siku saba.

Dkt Gwajima amesisitiza kuwa watakaokamilisha mapema na kwa ufanisi ndiyo watapewa fedha za awamu inayofuata ya mwaka 2020/21 na wasiokamilisha kwa wakati watakuwa na hoja ya kujibu na hatua stahiki zitachukuliwa.

Katika hatua nyingine Dkt Gwajima amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao kupitia Kamati za Uratibu wa ujenzi huu.