Mwenyekiti wa Desk & Cair Foundation, Alhaji Sibtain Meghjee wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazazi, walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana, Diwani na Mtendaji wa Kata ya Nyamagana wilayani humo baada ya kukabidhi vifaa vya mfumo wa maji tiririka kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi na walimu kunawa mikono kujikinga na corona.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyamagana akinawa mikono ikiwa ni ishara ya kupokea vifaa vya majitiririka vilivyotolewa na The Desk & Chair kwa a matumizi ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo kunawa mikono ili kujikinga na virusi vya corona.
Diwani wa Kta ya Nyamagana ( CCM Bhiku Kotecha akizindua mfumo wa kisasa wa maji tiririka uliofungwa na The Desk & Chair Foundation katika Shule ya Msingi Nyamagana ili kuwasaidia walimu na wanafunzi kunawa mikono kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona. Picha zote na Baltazar Mashaka
*******************************
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
SHULE ya Msingi Nyamagana iliyopo jijini Mwanza imepokea msaada wa vifaa vya mfumo wa majitirika kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi na walimu kujikinga na maambukizi ya virusi vya homa kali ya mapafu (Covid-19).
Msaada huo umetolewa juzi na The Desk & Chair Foundation (TDFC) ikiwa maandalizi ya wanafunzi kurudi shuleni kuendelea na masomo baada ya shule kufunguliwa na serikali ikiwa ni baada ya kufungwa kwa miezi mitatu kutokana na changamoto ugonjwa wa corona.
Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni mashine za mfumo wa maji tiririka Mwenyekiti wa TDFC Alhaji Sibtain Meghjee alisema mifumo hiyo (two touch free hand washing mashine ) ilimeunganishwa kisasa kwenye matenki ya ujazo wa lita 100 za maji kila moja kwa ajili ya wanafunzi 800 kuosha mikono na ndoo mbili za lita 20 za maji kwa matumizi ya walimu kunawa mikono.
“Huu ni mwendelezo wa taasisi yetu katika jitihada za kuwakinga na kuwalinda watanzania na maambukizi ya Covid-19 ambapo shule ya msingi Nyamagana leo inanufaika na vifaa vya mfumo wa maji tiririka kulingana na sera ya serikali ya elimu bure na pia shule hii imenufika na misaada wa kisima cha maji, madawati na vyoo vya walimu na wanafunzi .
Uongozi wa Shule hiyo ya Msingi Nyamagana ulishukuru taasisi ya The Desk & Chair kwa jitihada zake za kuunga mkono serikali katika kusaidia kutatua changamoto za elimu kwenye shule hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa Nyamgana (CCM) Bhiku Kotecha, alisema msaada huo umetolewa muda muafaka wa shule kufunguliwa na kuipongeza TDCF kwa kutambua, kujali na kuthamini afya na maisha ya watoto masikini wa Kitanzania hasa kipindi hiki cha kupambana na janga la corona