Home Mchanganyiko THE DESK & CHAIR YABADILISHA MAISHA YA FAMILIA YA MZEE BILAL

THE DESK & CHAIR YABADILISHA MAISHA YA FAMILIA YA MZEE BILAL

0

.Nyumba ya awali ya familia ya mzee Omari Bilal baada ya ukuta wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha kote nchini.

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Sibtain Meghjee (kulia) baada ya kumkabidhi nyumba Omari Bilal (kushoto).Nyumba hiyo yenye vyumba vitatu, sebule, choo, bafu na mfumo wa umeme jua imejengwa na taasisi hiyo kwa gharimu sh. milioni 15.
Picha na Baltazar Mashaka
******************************
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
NI VIGUMU kuamini lakini inawezekana baada ya familia ya mzee Omari Bilal, mkazi wa Nyamhongolo katika Manispaa ya Ilemela, kupata msaada wa makazi ya kudumu.

Familia hiyo hivi karibuni ilipata changamoto ya ukuta wa nyumba yao iliyojengwa kwa matofali ya tope kuanguka kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha mfululizo kwa miezi kadhaa na bahati nzuri hakuna madhara ya kibinadamu yaliyotokea kwenye familia hiyo.

Kutokana na changamoto hiyo Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TDCF) Tawi la Tanzania liliamua kujenga nyumba bora ya kuishi ya gharama nafuu  na kuikabidhi kwa familia hiyo.

Akikabidhi nyumba hiyo kwa  mzee Bilal, Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Sibtain Meghjee, alisema kuwa iliamua kubeba jukumu hilo baada ya kuguswa na changamoto ya familia hiyo kuwa katika hatari kuangukiwa na nyumba kwa sababu kuta zake hazikuwa imara baada ya upande mmoja kuanguka.

“Taasisi yeti ilichukua maamuzia ya kumjengea nyumba bora  ya gharam nafuu ya vyumba vitatu, sebule, jiko, bafu, choo na kufunga mfumo wa umeme jua.Nyumba hii imegharimu sh. milioni 15 tu ambapo ujenzi umekamilika na leo tunaikabidhi kwa familia hii iweze kujistiri na kuendesha maisha yao,”alisema.

Mwenyekiti huyo aliwashukuru wafadhili waliotoa msaada wa fedha zilizotumika kwenye ujenzi wa nyumba hiyo na kuiwezesha familia ya mzee Bilal kupata makazi bora ya kudumu na kuondokana na tishio la kuangukiwa na kuta za nyumba yao ya awali ambayo pia imekarabatiwa.

Kwa upande wake mzee Bilal aliushukuru uongozi wa The Desk & Chair kwa kujali na kutambua changamoto iliyokuwa ikiikabili familia yake na kwamba hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo wao wa huruma.

Aidha baadhi ya majirani wa familia hiyo Beata John na Paul Bubinza waliipongeza taasisi ya The Desk & Chair kwa jinsi inavyoshughulikia na kutatua matatizo ya jamii bila kubagua na kwamba familia hiyo ilikuwa kwenye mtihani mzito wa kuangukiwa nyumba lakini sasa maisha yamebadilika baada ya kukabidhiwa nyumba mpya ya kisasa