Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma akiwasili katika kuzindua mradi wa maji alioujenga kwa ahadi yake.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akitazama wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma wakicheza ngoma mara baada ya kuwazindulia mradi wa maji na kumaliza tatizo la maji.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji mradi huo umejengwa na yeye mbunge kwa ahadi aliyowapa mwaka 2015.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa juu ya mtambo akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma kwa kushirikiana naye ambapo amezindua mradi wa maji kwa ahadi yake na kumaliza tatizo la maji.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma kwa pamoja wakifurahia kwa kupata maji mradi ulitekelezwa na mbunge huyo kipindi cha kampeni mwaka 2015 na kumaliza tatizo la maji baada ya leo kuzindua rasmi kisima cha maji.
Sehemu ya akinamama wakichota maji mara baada ya Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kuwachimbia kisima cha maji Mradi uliotekelezwa na Mbunge huyo kipindi cha kampeni mwaka 2015.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma wakimshukuru Mhe.Mavunde kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwachimbia kisima na kumaliza kabisa tatizo la maji ahadi hiyo aliitoa kipindi cha kampeni mwaka 2015 na leo amezindua rasmi.
……………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ametekeleza ahadi yake ya kuwachimbia kisima cha maji wananchi wa kijiji cha Mayeto kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma.
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Akizindua uchimbaji wa mradi huo wa kisima, Mavunde amesema ameutafuta mradi huo kwa miaka minne iliyopita.
“Nilikuwa na uhakika nitachimba maji Mayeto baada ya kupitia mchakato wa kiserikali tuliona wananchi watapata changamoto ndipo iliponilazimu kutafuta ndugu zangu Ismail Kirito kutoka Tanga zaidi ya kilometa 600 ni Heshima kubwa wametupa kwani maji haya yatasaidia kaya mbalimbali na vizazi vijavyo,”amesema.
Ameongeza kuwa Kijiji Cha Mayeto ni cha pili katika mradi wa kuchimba kisima cha maji Kati ya visima vinne Mbalawala, Zuzu na Matumbulu.
“Lengo ni kuona wananchi wangu mnapata maji zaidi na kufurahia juhudi za serikali,”amesema.
Hata hivyo amepongeza juhudi za Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi Barabara ya lami ambayo itapita kwenda mkoani Arusha na itahamasisha kuimarisha uchumi zaidi katika Kijiji Cha Mayeto.
Wananchi wa kitongoji Cha Maheto wamemshukuru Mbunge na kudai kuwa kwa muda mrefu iliwalazimu kutembea kilometa nne hadi Kijiji Cha Mavundi kwa ajili ya kuchota maji na kusababisha wanawake kupata migogoro kwenye ndoa zao