Home Mchanganyiko TMDA YAZINDUA MKATABA MPYA WA HUDUMA KWA WATEJA LEO

TMDA YAZINDUA MKATABA MPYA WA HUDUMA KWA WATEJA LEO

0

Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi akikata utepe kuzindua mkataba mpya wa huduma kwa wateja kwa pamoja na Eric Shitindi Mwenyekiti wa Bodi ya TMDA kulia na Kaimu Mkurugenzi wa TMDA Bw Adam Fimbo kushoto hafla ya uzinduzi imefanyika ofisi za TMDA Mabibo jijin Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa TMDA Bw Adam Fimbo akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TMDA Bw. Eric Shitindi ili kumkaribisha mgeni rasmi.

Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mkataba huo uliofanyika kwenye ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es salaam leo.

Viongozi hao wakionesha mkataba wa huduma kwa wateja pamoja mara baada ya kuzinduliwa rasmi.

……………………………………………………..

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto imesema Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinapaswa kuwa na mkataba wa huduma kwa Wateja ili kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Hayo ameyasema Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi jijini Dar es Salaam wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamalaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), amesema kuwa TMDA imekuwa na mipango mizuri katika utoaji wa huduma kwa kuzingatia muda katika utoaji wa leseni kwa wadau mbalimbali.

Profesa Makubi amesema kuwa TMDA imekuwa na mifumo ya viwango ambapo Shirika la Afya Duniani inatambua pamoja na jumuiya mbalimbali na hiyo inatokana na mikakati ya watendaji wa taasisi waliojiwekea ya kuhakikisha wanakwenda kutatua matatizo ya huduma katika utoaji wa huduma.

Amesema kuwa TMDA inatoa mkataba mara ya nne ambapo amewataka mamlaka hiyo kufatilia mkataba huo kuona malengo waliojiwekea yameweza kama wameweza waliojipangia pamoja na huduma wanazozitoa kwa wadau.
Nae Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema kuwa katika mkataba huo wamezingatia muda wa utoaji wa usajili za waingizaji dawa kutoka siku 240 hadi 180 na wa ndani kutoka siku 120 hadi siku 60 na usajili dawa sehemu za biashara kutoka siku 10 hadi 8.

Fimbo amesema kuwa mkataba huo umezinagatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma na kuleta ufanisi pamoja na kuweka mikakati kuendelea kutoa huduma bora
kwa wadau
amesema TMDA tangu walipoanza kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja wamekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma bora kutokana na watendaji kujipanga katika kuhudumia wateja hao.