Cristiano Ronaldo na Paulo Dybala wakishangilia baada ya Juventus kupata bao la kwanza katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Lecce kwenye mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Allianz Jijini Torino. Mabao ya Juve yalifungwa na Paulo Dybala dakika ya 53, Cristiano Ronaldo dakika ya 62, Gonzalo Higuain dakika ya 83 na Matthijs de Ligt dakika ya 85 na kwa ushindi huo dhidi ya Lecce iliyocheza pungufu tangu dakika ya 32 kufuatia Fabio Lucioni kutolewa kwa kad nyekundu ya moja kwa moja kwa kucheza rafu mbaya, kikosi cha Maurizio Sarri kinafikisha pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kuongoza Serie A kwa pointi saba zaidi ya Lazio ambayo ina mechi moja mkononi PICHA ZAIDI SOMA HAPA