Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Bisahara Mhe. Mhandisi Stella akifunga mafunzo ya kwa maafisa biashara na tehama kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kuhakikisha wanawafikia wananchi wote katika kutoaji huduma ikiwemo kusajili Makampuni na Majina ya Biashara kwa njia ya mtandao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya ili kufunga mafunzo hayo leo.
Picha ya pamoja.
……………………………………………..
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Bisahara Mhe. Mhandisi Stella leo ameipongeza Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kutoa elimu kwa maafisa biashara na tehama kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kuhakikisha wanawafikia wananchi wote katika kutoaji huduma ikiwemo kuwasajili wafanyabiashara kwa njia ya mtandao.
Maafisa hao waliopewa mafunzo wametoka katika mikoa Mwanza, Mbeya na Mtwara ikiwa ni sehemu ya mipango ya brela ili waweze kwenda kuwafundisha maafisa wengine katika mikoa mbalimbali hapa nchini katika kutoa huduma.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo kwa maafisa biashara na tehama Mhe. Mhandisi. Manyanya, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kutoa huduma kwa uweledi ili waweze kuleta matokeo chanya kama serikali ilivyokusudia pamoja na kuepuka vitendo vya rushwa.
“Naomba brela kuendelea na mfumo huu wa kutoa elimu kwa maafisa biashara na tehama katika mikoa mengine i kuwafikia wananchi wote kwa ukaribu” amesema Mhe. Mhandisi Stella.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa amesema lengo la kutoa elimu kwa afisa biashara na tehama ili waweze kuwasajili wafanyabisahara jambo ambalo litawasaidia kupata takwimu sahihi katika maeneo yao.
Amesema kuwa baada ya kupata elimu hiyo maafisa hao watakwenda kuwa walimu kwa kuwafundisha maafisa wengine katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kwa upande wake Afisa Biashara kutoka Mkoani Mtwara Janeth Mhegelle, amesema baada ya kushiriki mafunzo hayo amekuwa na uelewa kwa kusajili kampuni na wafanyabishara kwa njia mtandao.
Amesema kuwa ni fursa kwa kwenda kuwafundisha maafisa wengine katika kuhakikisha watoa huduma bora kwa watanzania.