Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka (kulia) wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nachingwea,Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka (kulia) wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Sengeli, Hassan maarufu kwa jina la Dogo H. wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Mwimbaji wa nyimbo za Sengeli, Hassan marufu kwa jina la Dogo H akitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa, Juni 24, 2020. (
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………………………………………
*Awataka wakulima waendelee na kilimo katika kipindi hiki cha mpito
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa mazao mbalimbali ya biashara wakiwemo wakulima wa ufuta nchini waendelee na kilimo na kwamba suala la kushukuka kwa bei lililotokea kwenye msimu wa mwaka huu lisiwakatishe tamaa kwani jambo hilo litakwisha.
Amesema Serikali inaendelea kulifanyia kazi hilo na kwamba bei ya mazao nchini itaimarika baada ya kuongezeka kwa ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao nchini, ambapo wakulima watakuwa na masoko na uhakika na pia nchi itauza bidhaa zitokanazo na mazao hayo na si malighafi.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Juni 24, 2020) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Lindi alipokuwa katika ziara ya kikazina aliwasihi wakulima kutoacha kulima.
“Kushuka kwa bei ya ufuta kusiwakatishe tamaa na kuwafanya muache kulima kwa sababu bei haijashuka kwa zao hilo tu bali na mazao mengine kama chai, tumbaku, kahawa, chai na mazao mengine. Hali hii imetokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambao umeikumba dunia.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kadiri ugonjwa wa COVID-19 unavyoendelea kupungua katika Mataifa mbalimbali duniani hali bei ya mazao nayo itaimarika, hivyo wakulima waendelee kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho ni cha mpito.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi waje wawekeze katika viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali kwa sababu watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi pamoja na nishati ya kutosha.
Alisema moja ya msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuboresha sekta ya kilimo ili iweze kujitosheleza kwa chakula. “Suala la bei ya mazao linapangwa na wanunuzi Serikali inasimamia tu.”
Pia, Waziri Mkuu ameendelea kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa umoja na mshikamano mkubwa waliompatia katika kipindi chote cha miaka mitano na amewasisitiza waendelee na ushirikiano huo kwa ajili ya maendeleo ya wilaya yao na Taifa kwa ujumla.