Mikoa mengine inayopatikana kitabu hicho ni Arusha kupitia nambari ya simu: 0757690302, Morogoro kwa nambari ya simu 0659601522, huku mikoa kama Dodoma, Tanga na Mbeya ikitarajiwa kupokea kitabu hicho hivi karibuni.
Kitabu cha NIMEJITAKIA ambacho kimehaririwa na Bi Laura Pettie na kuhakikiwa na Mariam Mbano ni simulizi inayomhusu kijana Issa Matone. Kijana aliyefadhiliwa kisha kumlipa ubaya mfadhili wake.
Kijana huyo alipoamua kulichuma janga, hakutarajia janga hilo lingemshikia kiboko na kumcharaza vibaya mno. Lakini kitabu kinaonyesha namna Issa alivyoonywa, ila hakusikia. Hivyo yaliyomkuta, ni kama alijitakia. Ni simulizi yenye mafunzo lukuki ndani yake.
Katika kuhakikisha wasomaji nchini kote wanafikiwa na kujifunza kutoka katika Kitabu cha NIMEJITAKIA menejimenti ya mwandishi Mohammed Hammie imeandaa shindano lililopewa jina la Jitakie Na Ushinde lililozinduliwa rasmi leo kupitia mitandao ya kijamii hususani Facebook,unaweza kujua zaidi kuhusu shindano hilo kwa kutembelea kurasa za mtandao wa kijamii wa facebook kwenye ukurasa wa mwandishi Laura Pettie,Mariam Mbano,Hanifa Kafashe au mwandishi mwenyewe .
Hii ni riwaya ya pili kutoka kwa mwandishi Mohammed Hammie Rajab, riwaya yake ya kwanza ni ile ya YALIYONIKUTA TANGA, ambayo bado inafanya vizuri sokoni.
Mohammed ni mtoto wa aliyekuwa nguli wa uandishi nchini Tanzania, marehemu Hammie Rajab aliyewahi kutamba na riwaya kama Sanda Ya Jambazi, Kamlete Akibisha Mlipue, Somo Kaniponza, Ama Zangu Ama Zao, Balaa na nyengine nyingi.
Kwa shilingi 10,000/= tu za Kitanzania unajipatia kitabu cha NIMEJITAKIA ukajifunza na kuburudika vya kutosha.