Wananchi waliojitokeza kuhakiki majina yao baada y Tume kutoa orodha ya wananchi waliopoteza sifa ya kuwa wapiga kura.
picha na masanja mabula
**********************************
Na Masanja Mabula , Pemba.
TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar-ZEC-Wilaya ya Wete imetoa orodha ya wananchi waliopoteza sifa ya kuwa wapiga kura na kuwataka wananchi kwenda kuhakiki majina yao.
Afisa wa tume hiyo Wilaya ya Wete Issa Juma Hamad alisema aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kuhakiki ili taarifa zao ziweze kuingizwa kwenye daftari kwa walio na sifa ya kuwa wapiga kura.
“Inawezekana jina likaorodheshwa kimakosa, hivyo ni vyema mwananchi afike kwenye vituo vilivyo wekwa na Tume ili kuhakiki taarifa zao”alishauri.
Aidha alisema kwamba mwananchi ambaye anahisi kuwa na sifa anatakiwa kuwassilisha vielelezo vyake ikiwa ni pamoja na kitaambulisho cha mzanzibar mkaazi.
Baadhi ya wananchi waliofika kuhakiki taarifa zao n kukuta majina yao yamepachikwa , walishangaa kwani wanazo sifa ya kuwa wapiga kura.
Uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba idadi kubwa ya majina yaliotolewa na Tume ni wale ambao hawajapata vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi.
Hata hivyo wapo baadhi ya wananchi wanavyovitambulisho la majina yao yameorodheshwa kuwa ni miongoni mwa waliokosa sifa.
Fatma Khamis wa Shengejuu alisema bado hajapata kitambulisho kipya cha mzanzibar Mkaazi , na kuomba taasisi husika kuwapatia vitmbulisho ili waweze kutumia fursa yao kidemokrasia.
Naye Bikuu Juma na Khamis Aji wa jimbo la Kojani alisema ni vyema Tume ya waliomba majina hayo kupachikwa kila kwenye kituo cha kupigia kura ili wananch wengi waweze kuhakiki majina yao.
Mwisho.
picha .
Afisa wa Tum e ya uchaguzi wilaya ya wete Issa Juma Hamad akizungumza na wananchi waliofika kuhakiki majina katika ukumbi wa Jamhuri Wete.