Meneja Kilimo wa TBL Plc,Joel Msechu akiongea na wakulima wa mtama katika kijiji cha Bumbuta wilayani Kondoa mkoani Dodoma
Meneja Kilimo wa TBL Plc,Joel Msechu (Kulia) akikagua mtama uliovunwa mkoani Dodoma hive karibuni.
Mradi wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo.
Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Bw. Issa Dinya, mkulima na mkazi wa kijiji cha Bumbuta, kilichopo wilayani Kondoa, alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula.
Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77% na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake.
Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko.
Akiongelea mafanikio ya mradi huu, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.
Redman, alisema kwa sasa TBL Plc, inanunua asilimia 74% za malighafi yak kutengenezea bidhaa zake nchini na inao mkakati wa kuongeza zaidi katika miaka ijayo. TBL imenunua tani zaidi ya 9,000 za mtama kwa ajili za uzalishaji wa bia zake maarufu za Eagle na Bingwa. ”Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi” alisema Redman.
Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini “Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka.
Mnamo mwaka 2018,kampuni ya ABInBEV, iliweka mkakati wa kuwapatia ujuzi wakulima, kuwaunganisha na taasisi za kifedha hadi ifikapo mwaka 2025 “Kutokana na mkakati huu biashara yetu imewekeza kuwawezesha wakulima wadogo nchini Tanzania kupata huduma za Kilimo Uza-huduma inayowawezesha kupata taarifa za masoko,hali ya hewa,mbinu za kilimo cha kisasa kupitia ujumbe wa maneno kwenye simu zao,kupatiwa mikopo ya kilimo,mafunzo ya utawala wa fedha,huduma za ugavi wa mazao kwa kiwango bora,taarifa za tafiti za uendelezaji wa zao la mtama nchini Tanzania,mafunzo ya kuendesha kilimo cha kisasa wakati wote wa msimu,mbinu za kuendesha kilimo bora endelevu”alisema Redman.