Katibu tawala mkoa wa Kagera Prof.Faustine Kamuzora akiongea na maafisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba katika kikao kazi cha kujadili uboreshaji wa upatikanaji wa maji na vyoo bora katika vituo vya kutolea huduma.
Maafisa afya wa halmashauri za Manispaa ya Bukoba pamoja na halmashauri ya wilaya Bukoba wakimsikiliza Katibu tawala mkoa wa Kagera Prof.Faustine Kamuzora akiongea na maafisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba katika kikao kazi cha kujadili uboreshaji wa upatikanaji wa maji na vyoo bora katika vituo vya kutolea huduma.
Katibu tawala mkoa wa Kagera Prof.Faustine Kamuzora wapili kutoka kulia kwa waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na maafisa afya baada ya ufunguzi wa kikao kazi.
……………………………………………………………………………….
Na.Allawi Kaboyo,Bukoba
Katika kuhakikisha wananchi wanaendelea kujikinga na magonjwa ya mlipuko, Mkoa wa Kagera umepokea shilingi bilioni 1.9 kwa mwaka wa fedha unaomalizika juni 2020 kwaajili ya kuboresha upatikanaji wa maji na vyoo bora kati vituo vya kutolea huduma za afya.
Hayo yamesemwa leo juni 20 mwaka huu na katibu tawala wa mkoa huo Prof. Faustine Kamuzora wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha siku na maafisa Afya kutoka halmashauri za Bukoba na Manispaa mjini Bukoba ambapo ameeleza dhumuni la kupewa fedha hizo.
Prof. Kamuzora amesema kuwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ni eneo muhimu sana kusimamiwa asa katika kudhibiti magonjwa yanayoweza kuambukizwa pale mgonjwa anapokuwa katika vituo hivyo na kuongeza kuwa kwa kusimamia vizuri eneo hili wahudumu wa afya pia wataweza kujikinga.
“Eneo la ujenzi na matumizi ya vyoo ni eneo muhimu sana ambalo sisi wataalamu tunapaswa kulipa kipaumbele kwa sehemu kubwa katika ngazi ya jamii na vituo vya kutolea huduma, napenda kumshukuru Mhe.Rais Magufuli ambapo katika mwaka wa fedha unaoishia mwezi juni ametupatia kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwaajili ya kuboresha upatikanaji wa maji na vyoo bora.” Amesema Prof.Kamuzora.
Aidha Prof.Kamuzora amewaagiza mabwana afya na mabibi afya kutokaa ofisini na badala yake wasimamie shughuli zote za kinga katika maeneo yao ukiwemo ujenzi wa vyoo bora ngazi ya kaya na uwekaji wa sehemu za kunawia mikono mara baada ya kutoka chooni pamoja na uzoaji na utupaji sahihi wa taka.
Kwaupande wake afisa afya mkoa wa Kagera Ndg.Nelson Rumbeli amesema kuwa kwasasa mkoa huo una asilimia 57% ya vyoo bora na asilimia 99 ya aina yoyote ya vyoo hali inayopelekea uwepo wa asilimia kubwa ya upungufu wa magonjwa ya mlipuko.
“wagonjwa wengu wanaokuja katika vituo vyetu wanakuwa na matatizo ya magonjwa yanayotokana na uchafu, Katika kipindi hiki cha miezi mitatu ambayo watu wamekuwa wakinawa mara kwa mara magonjwa haya yamepungua kwa sipidi kubwa na ndo maana tumewaita hapa maafisa afya ngazi ya jamii na kata ili elimu watakayoipata hapa basi wakaitumie kuwaelimsha wananchi huko katika maeneo yao.” Amesema Nelson.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya Bukoba Dkt. Bandiot Gavyole ameeleza kuwa katika halmashauri yake kaya zenye vyoo bora ni asilimia 35% ambayo imeongezeka kutoka asilimia 30% kabla ya kuanza kwa kampeini ya nyumba ni choo na kuongeza kuwa kaya ambazo hazina vyoo ni kaya 91 sawa na asilimia 0.14%.