………………………………………………………………………………….
Na. Mwandishi wetu – OSG
Mahakama ya Afrika Mashariki leo tarehe 17 Juni mwaka 2020, imetupilia mbali maombi yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali kupinga kutumika kwa baadhi ya vifungu vya marekebisho ya Sheria ya Vyama Vya Siasa, Sura 258 ya Sheria za Tanzania.
Shauri hilo Na. 02 la mwaka 2020, lilifunguliwa katika Mahakama hiyo na Freeman Mbowe, Zitto Zuberi Kabwe, Hashimu Rungwe,Seif Shariff Hamad na Salum Mwalimu ili kupinga kutumika kwa baadhi ya vifungu vya Marekebisho ya Sheria ya mpaka pale shauri Na.3 la mwaka 2019 lililopo katika Mahakama hiyo litakapo sikilizwa na kutolewa uamuzi.
Walalamikaji katika shauri hilo pia walikuwa wakiiomba Mahakama hiyo kutamka wazi kuwa baadhi ya vifungu vya marekebisho ya Sheria ya Vyama Vya Siasa Na. 1 ya mwaka 2019 vinakiuka Mkataba uanzi.?? Kuhusu nini?? Wakivitaja Vifungu wanavyodai vinakiuka mkataba huo waleta maombi hao walivitaja vifungu hivyo kuwa ni kifungu cha 3 ambacho kimerekebisha kifungu cha 4 cha Sheria ya Vyama Vya Siasa, Sura 258 ya Sheria za Tanzania.
Viongozi hao wa Vyama Vya Siasa nchini walidai kuwa, vifungu vingine wanavyoomba viondolewe na Mahakama hiyo ni kifungu kidogo cha (5) (b) na (f) (2), (3), (4), (5) na (6) 5B (1), (2), (3), na (4) 6A (5) 6B (a), 8C (2), (3), na (4), 8E (i), (2), (4), na (5) pamoja na kifungu cha 23 ambacho kinarekebisha kifungu cha 18 (6), 12D na 21E cha Sheria hiyo.
Walalamikaji waliongeza kuwa pamoja na mambo mengine vifungu hivyo vinakiuka Ibara ya 6 (d) na 7(2) ya mkataba huo kwa kile walichoeleza kuwa Sheria hiyo ya marekebisho ya vyama vya Siasa ya mwaka 2019 itavilazimisha Vyama vya Siasa kutunga sera za vyama ambazo zitakuwa kinyume na itikadi, misingi na Imani za vyama hivyo.
Waliendelea kuieleza Mahakama hiyo kuwa kutumika kwa Sheria hiyo kutaondoa usawa kati ya vyama hivyo ikiwemo kunyimwa ruzuku sambamba na kuleta ubaguzi miongoni mwa wananchi ambao mzazi wao mmoja si mtanzania. Baada ya upande wa Serikali kupokea maombi hayo, Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali waliweka pingamizi Mahakamani kwa lengo la kupinga shauri hilo kwa kupeleka hoja tatu ambazo zilikubaliwa na Majaji wote watatu waliosikiliza shauri hilo.
Wakiwasilisha hoja hizo mawakili wa Serikali wakiongozwa na WAkili Wa Serikali Mkuu Bi. AleSia Mbuya waliiomba Mahakama hiyo kulitupilia mbali maombi hayo kwa kuwa hayakuwa na msingi wowote wa kisheria. Mawakili wa Serikali waliieleza Mahakama hiyo kuwa kutumika kwa vifungu hivyo vya Sheria ya Vyama vya Siasa hakutakuwa na madhara yoyote kwa wananchi hususani wanachama na viongozi wa vyama vya siasa.
Aidha waliieleza Mahakama hiyo kuwa hakuna sababu kwa Mahakama hiyo kuzuia kutumika kwa sheria hizo kwa kwa wakati sheria inayolalamikiwa ilikuwa tayari imeanza kutumika wakati shaurinli;I;ofunguliwa na kuwa na hakukuwa na malalamiko miongoni mwa watumiaji kwa kuwa elimu kuhusu matumizi ya Sheria hiyo ilitolewa . Seikali ilibainisha kuwa, kuzuia matumizi ya sheria hiyo kutapelekea kuwanyima wananchi fursa ya kimsingi ya kuishi kwa kufuata sheria na taratibu kwa mujibu wa Katiba.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki wakiongozwa na Mhe. Jaji Monica K. Mugenyi walikubaliana na hoja za upande wa Serikali hatua iliyopelekea kuyatupilia mbali. Majaji wengine waliosikiliza shauri hilo ni pamoja na Mhe. Jaji. Dkt. Fausine Ntezilyayo, Mhe. Jaji. Audace Ngiye, Mhe. Jaji Charles O.Nyawello pamoja na Mhe. Jaji Charles Nyachae.
Shauri hilo lililoendeshwa kwa njia ya mtandao, upande wa Serikali umewakilishwa na Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bi. Alesia Mbuya, mawakili wa Serikali Bw. Yohana Marco, Bi. Vivian Method na Bw. Stanley Kalokola wakati upande wa walalamikaji waliwakilishwa na Mawakili wa kujitegemea Bw. John Mallya pamoja na Bw. Jebra Kambole