****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa amesema kuwa serikali itawachukulia hatua wafanyabiashara wote wa mafuta walioficha nishati hiyo na kuacha kuuza kulingana na bei elekezi.
Waziri Bashungwa ametoa onyo hilo wakati wa kikao cha pamoja na mamlaka zinazosimamia kodi (TRA) , Nishati (EWURA) na Tume ya Ushindani (FCC) kujadili sababu na hatua zitakazochukuliwa kwa wafanyabiashara watakaobainika kwenda kinyume na sheria.
Amesema kutokana na janga la Covid-19 bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka huku ikichangiwa zaidi na mkakati uliowekwa wa ununuaji wa mafuta kwa pamoja, ambapo pia ametaja sheria zitakazotumika kuwakamata wanaoficha mafuta.
Pamoja na hayo Mhe.Bashungwa amezitaka tume ya ya ushindani FCC, pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA, kutumia sheria kuwaadhibu wafanyabiashara ambao hawajashusha bei za mafuta licha ya kushuka kwa kiasi kikubwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA Bw.Godfrey Chibulunje ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA, amewataka wauzaji wa mafuta ya reja reja kutoa taarifa za watu kukataa kuwauzia mafuta kwa wakati huu kwa lengo la kuyatunza hivyo kuweza kuwachukulia hatua kwa kushindwa kutekeleza leseni zao.
Kushuka kwa bei ya mafuta nchini na Duniania kwa ujumla kunatajwa kusababishwa na kuwepo kwa mripuko wa ugojwa wa covid 19 hivyo kusabisha mafuta kutokutumika kama awali kwani matumizi yake yamepungua kutokana na shughuli za kibinadamu kupungua